BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UFARANSA YAFICHUA SIRI KUANGUKA KWA NDEGE YA ABIRIA YA MH17 YA SHIRIKA LA NDEGE LA MALAYSIA NA KUPOTEZA UHAI WATU 298.

http://beforeitsnews.com/mediadrop/uploads/2014/30/500b38999098f7a4455e6b8931afbb57f892eaf1.jpg
Ndege ya MH17 ya Malaysia ilidunguliwa.

Muombolezaji akiweka saini kama ishara ya kutoa pole zake kwa waathiriwa.
Wachunguzi wa Uholanzi waliokuwa wanachunguza chanzo cha ajali ya ndege ya Malaysia nchini Ukraine mwezi Julai wanasema kuwa ndege hiyo ya abiria ilikumbwa na kitu chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali.

Mwandishi wa BBC amesema kwamba ushahidi huo ni wa wazi na kwamba ndege hiyo ilishambuliwa kwa kombora.

Katika ripoti yao ya kwanza ya kiuchunguzi ,maafisa hao wa Uholanzi wanaojihussha na masuala ya usalama wa anga wameeleza kua hapakuwa na tatizo la kiufundi lililosababisha ndege hiyo ipate ajali, ama makosa ya rubani yalosababisha ndege hiyo kulipuka.

Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurekodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.

Abiria wote miambili na tisini na nane walipoteza uhai pindi ilipoanza safari kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala Lumpur.Kutokana na ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua ndege hiyo.

Lakini mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na ajali hiyo.

Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 itatolewa mwakani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: