Hili ni gari lingine ambalo lenye usajili namba T397ANU nalo lilihusika katika ajali hiyo leo.
Moja ya gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamadi baada ya kupata ajali, Misungiwi, Mwanza.
Keria ya moja ya magari yaliyopata ajali ikiwa chini baada ya kufyatuka baada ya ajali.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia msafara wa Maalim Seif, mara baada ya ajali.
Msafara wa Maalim Seif ukijiandaa kuondoka mara baada ya magari mawili kati ya saba yaliyokuwa kwenye msafara kupata ajali.
Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando (kulia) na muonekano wa gari (kushoto) baada ya ajali katika wilaya ya Misungwi, jijini Mwanza.
Mkuu wa kitengo cha habari Wilaya, Mh Shido ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtaa Utemini Kata ya Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando.
Akizungumza na mtandao huu, Mkurughenzi wa Habari wa CUf, Adam Kambaya alisema Viongozi wawili wa CUF, katibu wa wilaya ya Nyamagana na mwenyekiti wa mtaa wa Nyamagana ambao hakuwataja majina wamelazwa katika Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.

0 comments:
Post a Comment