Mwandishi wa StarTV Morogoro, Jackson Monela naye akiangalia.
Mwandishi na mpiga picha wa kituo cha ITV Morogoro, Hussein Nuha akichungulia katika darubi iliyofungwa katika silaha aina ya fifle 0.308 ili kuona mbali wakati wa maonyesho wa vifaa vinavyotengenezwa na shirika hilo katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOGMeneja wa Shirika la Mzinga, Meja Jenerali, Dk Charles Muzanila kulia akimuonyesha Bendera mashine ya kufanyia mazoezi ambayo yanasaidia kupounguza kitambi kwa muda mfupi.PICHA/MTANDA BLOG.
Mtanda Blog,Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera amesema uamuzi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere kuanzisha Shirika la Mzinga, umeliwezesha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kutekeleza majukumu yake bila kuwa tegemezi wa kuagiza vifaa vingi vya kijeshi kutoka nje.
Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 40 ya Shirika la Mzinga Septemba 10 mjini hapa, Bendera alisema uamuzi huo wa Mwalimu, umeleta tija kubwa kwa jeshi na taifa kwa jumla.
Mkuu huyo wa mkoa, alisema shirika hilo limekuwa mkombozi kwa vikosi vya kijeshi hapa nchini kutokana na uwezo wake katika kuzalisha vifaa vya kijeshi na hata vya kiraia.
“Katika maadhimisho haya, tuna cha kujivunia si kwa upande wa jeshi tu bali hata kwa wananchi, maana nao wananufaika na kazi zinazofanywa na Shirika la Mzinga,” alisema Bendera.
Pamoja na vifaa vya kijeshi, shirika hilo pia linatengeneza samani za ofisini na majumbani, vipuri vya magari na mitambo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya raia.
“Lakini pia Mzinga wanazalisha risasi za shotgun, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, mashine za kukamulia mbegu za mafuta, mashine kuranda mbao na kufyatulia matofali, haya ni mafanikio makubwa,” alisema mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake, Meneja wa Shirika la Mzinga, Meja Jenerali, Dk Charles Muzanila alisema tangu miaka ya 1990 shirika lilianza kuagiza na kusimika mitambo mipya kwa ajili ya uzalishaji wa risasi za kiraia za shotgun na breaki za treni za Shirika la Reli Tanzania.
“Baadaye, shirika liliandaa mkakati wa maendeleo wa miaka mitano wenye lengo la kuliingiza shirika katika uzalisha wa mazao ya kibiashara na kuboresha msingi wa mazao ya kijeshi ili kujiingizia mapato na kupunguza ruzuku ya serikali.” alinena Dk Muzanila
Alisema chini ya mpango huo, shirika limeanzisha Kampuni Tanzu ya Mzinga Holding, litakalokuwa na jukumu la kuanzisha na kuendesha shughuli za biashara.
0 comments:
Post a Comment