NAMNA YA KUPATA MTOTO ENDAPO WATU WAWILI WANAISHI NA VVU, WATAHITAJI KUPATA ELIMU HII ILI MTOTO ASIPATWE NA MAAMBUKIZI.
Endapo watu wawili wanaoishi na VVU wamekubaliana kuishi pamoja kama mke na mume na wanatumia kondomu wanawezaje kupata watoto ?.
Hii ndio njia bora ya kufanya
Endapo wewe na mwezi wako mnaishi na VVU, haina maana kuwa ni mwisho wa ndoto zenu za kuwa na familia. Hata hivyo inaweza ikawa vigumu zaidi katika kufanya maamuzi.
Kwa hiyo, ni muhimu kuanza mchakato baada ya kupata habari na ufahamu wa kutosha na kwa kiasi kikubwa. Ni bora kusubiri na kufanya kile ambacho ni sahihi kuliko kuhatarisha afya ya mtoto wenu mtarajiwa.
SOMA MAKALA HII PIA: FAHAMU VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO (PMTCT).
Hapo nyuma, idadi kubwa ya watoto waliozaliwa na kinamama wanaoishi na VVU waliambukizwa VVU kutoka kwa mama. Lakini leo hii hali ni tofauti na nzuri zaidi kwa sababu kinamama wajawazito wanaweza kupata dawa madhubuti (dawa za kufubaza VVU yaani ARV’s), za kuzuia uambukizo wa VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
JE, UMESOMA MAKALA HII: SWALI: MIMI NI MJAMZITO, JE KAMA NIMEAMBUKIZWA VVU MTOTO ALIYE TUMBONI ANAPATAJE VVU?
Dawa hizi zikisaidiana na matibabu sahihi ya mtoto mchanga, kwa kiasi kikubwa zinaweza kupunguza hatari ya kupata mtoto asiyeambukizwa VVU. Kina mama wajawazito wanaoishi na VVU 98 kati 100 waliopata matibabu sahihi ya dawa za kufubaza VVU wanapata watoto wenye afya.
Ikiwa mmoja au wote wawili mnaishi na VVU, na mnatarajia kupata mtoto ni muhimu kumuona dakitari wenu ili awashauri kabla mama hajabeba ujauzito.
Dakitari atawashauri namna ya kupunguza hatari ya ninyi wawili kupata maambukizi mapya na ya kumuambukiza mtoto wenu mtarajiwa.
Kutokana na kuweko kwa uwezekano wa kumuambukiza mtoto kutoka kwa mama anayeishi na VVU kwenda kwa mtoto mtarajiwa, baadhi ya wenzi wangeweza kuchagua njia mbadala kama vile kuamua wasizae kabisa, bali wafanye utaratibu wa kuchukua mtoto wa kulea. Kwa habari zaidi tembelea http://www.manyandahealthy.com
0 comments:
Post a Comment