BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS JAKAYA KIKWETE AITWA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI.


JK.

Wadaiwa hao watawasilisha majibu kabla ya Novemba 7 mwaka huu na kutoa maelezo ya ziada Novemba 14 mwaka huu kabla ya Mahakama kupanga siku ya shauri hilo kusikilizwa na pande zote zitapewa wito maalumu.

Arusha. Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa mashahidi wanaotarajiwa kuitwa na walalamikaji katika shauri dhidi ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda linaloendelea katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).


Wakili Jimmy Obeid anayewawakilisha walalamikaji katika shauri namba 9/2013, jana aliieleza Mahakama kuwa miongoni mwa mashahidi watakaoitwa kujenga kesi hiyo ni pamoja na Rais Kikwete.


Shauri hilo lilifungulliwa na Watanzania watatu, Ally Hatib Msangi, David Makatha na John Bwenda wakidai kitendo cha Kenya, Uganda na Rwanda kufanya vikao bila kuzishirikisha Tanzania na Burundi ni ukiukwaji wa mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)


Miongoni mwa vifungu vya mkataba wa EAC vinavyodaiwa kukiukwa ni namba 3(3) (c) kinachotaka ushiriki sahihi kuimarisha ushirikiano ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kifungu cha 6 (a) (b) (d) na (f) kinachozitaka nchi wanachama kuzingatia misingi ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.


Katika ushahidi wake, Rais Kikwete ataombwa kuthibitisha hotuba yake kwa Taifa aliyoitoa bungeni Novemba 7, mwaka jana ambayo ilielezea jinsi Tanzania na Burundi zilivyotengwa na baadhi ya nchi wanachama wa EAC.


“Kutokana na uzito na majukumu ya Rais Kikwete tunayepanga kumwita kama mmoja wa mashahidi wetu, naiomba Mahakama muda wa mwezi mmoja kuwasilisha orodha ya mashahidi na hati za viapo,” alisema Obeid. Jopo la majaji watano wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Jean-Bosco Butasi, Naibu Jaji Kiongozi, Isaac Lenaola na wengine Faustin Ntezilyayo, Monica Mugenyi na Fakhi Jundu walikubali ombi hilo na kupanga Oktoba 24, mwaka huu wadai kuwasilisha hati ya kiapo na orodha ya mashahidi.


Wadaiwa katika shauri hilo ni Katibu Mkuu wa EAC, anayewakilishwa na wakili Dk Antony Kafumbe wakati mdaiwa wa pili ni Mwanasheria Mkuu wa Kenya anayewakilishwa na mawakili wawili, Muthoni Kimani na Peter Ngumi, mdaiwa wa tatu ni Mwanasheria Mkuu wa Uganda anayewakilishwa na mawakili watatu, Elisha Bafirawala, Richard Adrole na Maureen Ijang’ na mdaiwa wa nne ni Mwanasheria Mkuu wa Rwanda anayewakilishwa na wakili Malaala Aimable.


Wadaiwa hao watawasilisha majibu kabla ya Novemba 7 mwaka huu na kutoa maelezo ya ziada Novemba 14 mwaka huu kabla ya Mahakama kupanga siku ya shauri hilo kusikilizwa na pande zote zitapewa wito maalumu.


Septemba 2, mwaka huu, wadai waliondoa mahakamani ombi la zuio la muda dhidi ya vikao vya muungano wa wenye nia (coalition of the willing), baada ya Tanzania na Burundi kuanza kushirikishwa kwenye vikao viwili vilivyofanyika Februari 24 na Mei 2, mwaka huu.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: