BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KAGERA, NI TUHUMA ZA KUKODIWA NA KUFANYA MAUAJI IKIHUSISHA IMANI ZA USHIRIKINA.


Mmoja wa waganga wa tiba za ajili akifanya shughuli za uganga.Picha ya Maktaba.


POLISI mkoani Kagera, inashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukodiwa kufanya mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, alidai kwamba uchunguzi wa jeshi hilo, umebaini watuhumiwa hao wamekuwa wakikodishwa na watu mbalimbali kufanya mauaji na kupewa ujira wa kazi hiyo.

Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Maxmilian PhilMathias (25), Mkombozi Michael (40), Tumaini Basisili (27) na Buhu Mtunzi (34), wote wakazi wa wilayani Biharamulo.

Hata hivyo Kamanda Mwaibambe amesema makazi hayo si ya kudumu kwani wamekuwa wakihamahama mara kwa mara.

Alisema watu hao walikamatwa Septemba 10 mwaka huu, saa sita usiku huko Biharamulo kutokana na msako uliofanywa na jeshi la polisi baada ya kupata taarifa za kiintelijensia.

Imeelezwa kuwa wauaji hao walikuwa wakifanya mauaji hayo katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita na Simiyu pia walihusika na tukio la bibi kizee moja aliyeuawa Aprili mwaka huu wilayani Biharamulo.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: