BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FRIENDS RANGERS KUENDELEZA WIMBI LA USHINDI MBELA YA JKT MLALE LIGI DARAJA LA KWANZA ?.

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/08/AKIBIR-BABU-CHINI-PAUL-BARNABAS-POLISI-CENTRE-KUSHOTO-NA-ALEX-ATHANAS-BUKINA-FC-KULIA-LIGI-DARAJA-LA-KWANZA-JAMHURI-MORO-PIX-NO-3.jpg 
KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, yenye makazi yake Magomeni Kagera Dar es Salaam, kesho kinashuka kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuvaana na timu ya JKT Malale Mkoani Ruvuma,katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza.

Timu hizo zinacheza mchezo wao watatu huku Rangers ikiingia
dimbani na pointi 6, ilizopata katika mechi zake mbili ilizocheza.

Ofisa Habari wa timu hiyo Friends Rangers, Asha Kigundula,
amesema wamejipanga vizuri kushinda mchezo huo wa tatu licha ya
kutambua katika mechi kuna matokeo ya aina tatu.

Kigundula alisema kuwa kikosi chao chini ya kocha wao Mkuu Ali Yusuph
Tigana, kinawaomba wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi
kuishangilia timu yao, iweze kupata matokeo mazuri.

Alisema kuwa kujitokeza kwa mashabiki kutaipa nguvu zaidi timu yao, ambayo imejipanga kuhakikisha inapanda daraja msimu ujao na kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Nomba wapenzi wa Friends Rangers kutoka kona sehemu zote za mkoa wa Dar es Salaama, ikiwa ni pamoja na maeneo ya jirani kama vile Magemeni Kagera, Mwembe Chai, Manzese, Ubungo na
Magomeni"alisema Kigundula.

Alisema kuwa kila mchezaji ana hali kubwa ya kushinda mchezo huo
ili ijiweke vizuri.

Friends Rangers imeshinda mechi mbili ambapo mechi ya kwanza dhidi ya Lipuli, ambapo ilipata ushindi wa mabao 2-1, wakati mechi yake ya pili ilicheza dhidi ya African Lyon, ambapo ilishinda bao 1-0, mechi zote zimechezwa Uwanja wa Karume.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: