Na Juma Mtanda, Morogoro.
Ni safari iliyojaa kila aina ya adha ya usafiri wa shida kutoka Ifakara hadi Chita, ni safari ndefu ya wiki mzima ili kwenda katika kijiji cha Merela lengo likiwa kufuatilia suala zima la kutaka kujua ukweli juu ya wajawazito kujifungulia njiani tena kwenye mitumbwi wakati wakielekea katika zahanati ya kijiji cha Chita tarafa ya Mngeta wilaya ya Kilombero kufuata huduma za afya Morogoro.
Kijiji cha Chita kiko umbali wa kilometa 110 kutoka makao makuu ya wilaya ya Kilombero yaliyopo Ifakara, wilaya iliojaa neema ya zao la mpunga na samaki wa kila aina kutoka mto Kilombero ukiachilia neema nyingine mkoa wa Morogoro.
Mbali ya umbali wa kilometa 110 kutoka Ifakara-Chita itakulazimu kutembea kilometa 10 za ziada ili kufika katika kijiji cha Merela ambapo wananchi wake hutumia masaa matatu kipindi cha masika kufuata huduma za afya huku shida za kila aina zikiwakumba, wanafunzi wa sekondari, wajawazito, wagonjwa na wale wenye kutafuta mahitaji muhimu kijiji cha Chita.
Mwendo wa kuelekea kijiji cha Merela kwa masika ni mwendo wa masaa matatu kwa 85% ukiwa majini.
Kimahesabu safari ya kwenda Merela ukitokea Chita ama yule anayetembelea kijiji hicho ni lazima atembee kwa miguu saa 2:45 katika maji wakati katika mtumbwi ukitumia saa 1 na sehemu ya nchikavu kwa kutumia dakika 15 ndipo ufike katika kijiji, iwe unatokea Chita kwenda Merela au Merela kwenda Chita.
Ni adha ya namna gani ambayo utakumbane nayo katika safari ya kwenda Chita ili upate fursa ya kuianza safari ya kwenda Merela kwa kipindi cha masika ?, jibu ni rahisi tu ! na utaanza kulipata Ifakara eneo la mzunguko wa magari ambako ndiko magari ya kwenda Chita-Mlimba huegesha hapo na kuanza safari ya kwenda kijiji utakacho iwe Mbingu, Mngeta, Chita na hatimaye Mlimba ambako ni mwisho wa magari yanayotoa huduma kwa umma.
Eneo la mzunguko wa magari Ifakara kipindi cha masika eneo hilo hugeuka feli au eneo la kivuko kwa maana ya kuweka nanga mitumbi, boti, meli na vyombo vingine vya majini ikiwa tofauti yake eneo hilo panajulikana hivyo kwa sababu wananchi kuvushwa kutumia mkokoni na makundi ya vijana waliojitafutia ajira halali ya kuvusha watu kutoka daraja la mto Lumemo hadi katika mzunguko huo kwa ujira wa sh5,00 kwa mtu mmoja kutokana na mto huo kumwaga maji katika makazi ya watu na barabara kuu ya Ifakara-Mlimba.
Maji hayo yakielekea katika mto Kilombero katika utaratibu usio rasmi ambapo kwa hilo pekee litakuwa jibu tosha kuwa safari ya kwenda Merela ambako nako kuna adha nyingine utakutana nayo ya kukaa mkao mmoja tu katika mtumbwi tena wa saa 1 ili usiweze kumyumbisha mwendesha mtumbwi ili usije kupinduka kutokana na mitumbwi kuwa midogo ikilenga zaidi kwa matumizi ya uvuvi kwa kuvulia samaki katika mto Kihansi na maji yaliyosambaa zaidi ya kilometa 10katika bonde la mto huo.
Vikwazo vingine katika safari hiyo ikiwajumuisha wasafari wote kwa kipindi cha masika inayosababishwa na uharibifu wa miundombinu ya barabara kwa magari kukwama katika maeneo makuu ya Mbingu, Londo-Vigaini, Idete magereza, Kimbe na sehemu nyingine ndogo ndogo ambazo miundombinu imeharibiwa namaji ya mvua kwa kifusi kilichowekwa barabarani kushindwa kuendana na kasi na hali ya masika.
Hali hiyo imesabaisha kukwama kwa magari hata yale yenye uwezo wa nguvu yaziada (for wheel dreva) ikihusisha matrekta ambayo yanasifika kupita eneo lenye vikwazo vigumu vya barabara na kuchangia wasafiri kutozwa nauli kati yash25,000 hadi sh30,000 badala ya sh15,000 hadi sh20,000 kwa wale wa Mlimba huku pikipiki ikitoka kiasi cha sh45,000 kwa Ifakara-Chita wakati Ifakara-Mlimba ikiwa ni kati ya sh70,000 bei hizo zinatokana na ubovu wa barabara hiyo ama unaweza kutozwa zaidi ya kima hicho.
Naanza safari ya kutoka Morogoro mjini kwenda Merela april ambapo ijumaa yaapril 18 mwaka huu kwa usafiri wa pikipiki kutoka Ifakara-Chita baada ya kutoka ule wa gari kutoka Morogoro-Ifakara ilinipa picha hali ya ninakoenda kuona shida, taabu, karaha na kila aina ya usumbufu hasa ya kunondoka katika majiwakati naelekea Merela na Diwani wa kata ya Chita, Hassan Kidapa.
Tulianza safari kutoka Chita kuelekea Merela majira ya saa 5 asubuhi huku mvua ikinyesha baada ya kusubiria inyamaze lakini tukaona ni bora kuanza safari na hali hiyo na kutembea kwenye maji usawa wa kiunoni, magotini na kifundo cha mguu na kutembea seheme chavhe za nchikavu kabla ya kuufikia mtumbwi kutufikisha kijijini Merela.
Katika mitumbwi hiyo ni midogo ikitengenezwa kwa ajili ya uvuvi na sio kwa ajili ya kusafirisha abiria hivyo kukulazimu abiria kukaa kama mzigo kuepuka kutingishika mtumbwi huo kuyumbisha na kufika salama safari yenu.
KAIMU AFISA MTENDAJI KIJIJI CHA MERELA.
Wa kwanza kuongea naye katika kijiji cha Merela kata ya Chita tarafa ya Mngeta wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro ni Kaimu Afisa Mtendaji, Abdom Undole anaeleza kwa ufupi historia ya kijiji hicho.
Kijiji cha Merela kina vitongoji vya Idunda, Kalihanya, Kitundu, Ipungahewa na Msita ikiwa na zaidi ya wakazi 7960 na kaya zaidi ya 1,200 huduma muhimu zikitegemea kijiji cha Chita kama huduma za kiafya n:k.
Kuna zahanati imeanza ujenzi wake tangu 2010, boma likijengwa kwa nguvu yawananchi huku serikali ikitoa kiasi cha sh30 mil kwa ajili ya kumalizia. Alisema Undole.
Undole alisema kuwa kutokana na kuwa na vitongoji vitano katika kijiji hicho cha Merela ina mpango wa vitongoji viwili kuwa vijiji kamili kikiwemo kile cha Msita ambacho tayari kimeanza ujenzi wa shule ya msingi ikiwa na darasa mawili huku kikinge kikiwa katika matayarisho ili kupunguza umbali wa manafunzi kutembea kwa muda mrefu.
Kijiji hicho kimejaliwa kuwa na neema ya kuwa na kitoweo cha samaki aina mbalimbali ikiwemo kambale, pelage, kitoga na wengine hilo limetokana na kuzungukwa na mito mikuu ya Kilombero, kihansi, mpanga na mtondole huku samaki hao wakiuzwa mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Makambako na vijiji vya jirani wakisafirishwa kwa njia ya reli ya tazara.
Akielezea maisha ya wakazi wa kijiji hicho, Undole alisema kuwa Merela kinakabiliwa na changamoto kubwa hasa ile ya usafiri wa kutoka Chita hadi Merela hiyo ikisababisha kukosekana kwa barabara ya uhakiki ambayo ingesaidia kupitika nyakati zote za masika na kiangazi.
“Hatuna barabara ya uhakika wakati wa masika kwani usafiri wetu 85% ni kusafiri katika maji na nyakati za kiangazi ndio tunapata fursa ya kutembea kwa magari na pikipiki kwa kusafirisha wagonjwa na wananchi wenye kuhitaji mahitaji muhimu kijiji cha Chita ama kwenda Mlimba na Ifakara.”alisema Undole.
Aliongeza kwa kusema kuwa shida ya usafiri huo, wanaoathirika zaidi ni akinamama wajawazito wakiwemo wale wa jamii ya wafugaji ambao wamekuwa wakiathirika zaidi pindi wanapoelekea kujifungua katika zahanati ya Chita kutokana na kushindwa kutambua kalenda za nyakati za kujifungua.
Undole alisema kuwa adha hiyo itapungua pindi zanahati ya Merela itakapokamilika ujenzi wake na kupatiwa wataalam miezi ya baadye ama serikali itapoanza ujenzi wa barabara kwa kuweka matuta, madaraja na makaravati.
Kumekuwa na vifo kwa wagonjwa pindi wanaposafirishwa wakati wa masika kwa kutumia mitumbwi kwa mgonjwa kuzidiwa huku wengine wakipoteza maisha njia wakati wakielekea hospitali ya Ifakara, kituo cha afya Mlimba ama zahanati ya Chita ambako ni lazima kutumia usafiri huo wa mtumbwi kufika Chita ambako huo kupata usafiri wa gari.
Kwa mwaka 2012-2013 pekee wastani wa wagonjwa watano hujifungulia katikamitumbwi na wajawazito watano hufariki dunia na bidhaa za dukani kutumbikia mto kihansi.
“Matukio yaliyojitokeza katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2013 kuna vifo vya watu watano wamepoteza maisha na wajawazito kwa idadi hiyo wakijifungulia vichanga katika mitumbwi kutokana na adha ya usafiri nyakati za masika na mtoto kuporoshoka mgongoni mwa mama yake na kutumbikia kwenye majilakini aliokolewa.”alisema Undole.
HISTORIA YA KIJIJI CHA MERELA TANGU MWAKA 1975.
Marthin Chogo (68) anaeleza historia kamili ya kijiji cha Merela na kueleza kuwa kijiji hicho ni cha asili kikihasisiwa kabla ya 1945 na mwaka huo wananchi wakijiji hicho serikali iliwahamisha kutoka hapo na kwenda Ngombo wakati huo ikiwa ni wilaya ya Ulanga kabla ya kugawanywa ambapo baadaye miaka michache walirejea tena kijiji hapo.
Kuhamishwa kwa wananchi wa Merela kwenda kijiji cha Ngombo kulitokana na eneo hilo kuwa na mbung’o wengi na serikali ikihofia wananchi wake kupata magonjwa ya kuambukizwa na wadudu hao waliokuwa wakizaliana kwa wingi ambapo kurejea kwa kulizingatia masharti ya kupunguza miti. Alisema Chogo.
Kijiji hiki cha Merela kilifikiwa na wamisional kabla ya miaka ya 1930 wakieneza dini ya kikristo kwa wananchi na kujenga majengo mbalimbali ikiwemo kanisa na mwaka 1945, serikali ilipotoa amri ya wananchi kuhamishwa na wao walihama kwenda Ngombo na mwaka 1950 walirejea tena Merela. Alisema Chogo.
“Nilipata historia hiyo kutoka kwa mzee Pinga Pinga ambaye kwa sasa ni marehemu na mwaka 1950 hadi 1960, wananchi walikuwa wakipata huduma muhimu hasa bidhaa kutoka kutoka kwa uongozi wa kanisa la romani katoliki ambao baada ya wiki walikuwa na kawaida ya safiri kwa mtumbwi kufuata bidhaa Ifakara ukipita mto Kihansi kisha Kilombero na kusaidia kusafirisha wagonjwa.”alisema Chogo.
Wamisional hao pia walitengeneza daraja la miti katika mto Kihansi ili kuweza kuvuka kutoka Merela hadi Chita ili kwenda Mlimba, Mpanga na Taweta katikashughuli zao za kihoro na wananchi kufaidika na uwepo wao.
Mwaka 1971 reli ya tazara ilijengwa na wananchi wa kando ya reli walifaidika na usafiri huo huku mitumbwi ya kanisani iliyokuwa na injini ikianza kuchakaa ambapo daraja la mto kihansi na lenyewe likisombwa na maji kipindi cha masika mara kwa mara kabla ya miaka ya hivi karibu kujengwa daraja imara.alisema Chogo.
Chogo anatanabaisha matatizo ya chungu mzima kutokosekana kwa miundombinu ya barabara ya uhakika kwa wakazi wa Merela kwenda Chita kuwa ni pamoja na usumbufu wa kutumia mtumbwi kama njia kuu ya wao kutumia kama njia pekee ya usafiri wa majini nyakati za masika si kama serikali ikifanya makusudi kuweka tuta, madaraja, makaravati ili maji yafuate mikondo ya majikatika mto kihansi.
“Kupitisha mazao, matatizo ya wagonjwa, wajawazito kujifungulia njiani kama kwenye mitumbwi, wananchi kusafiri na bidhaa kutumbukia majini hii kero inaweza kutoweka kwa serikali kutengeneza barabara hilo litasaidia wananchi kuondokana na adhabu nyakati ya masika.”alisema Chogo.
Kero, shida, tabu na karaha maisha kuyaweka mkononi katika kipindi cha masika ni mabaya nao sio kwa akina mama kujifungulia njia bali hata wanafunzi wasekondari nao matatizo hayo yanawakumba wanafuata mahitaji kila kijiji cha Merela baada ya wazazi kuwapangia vyumba watoto wao ambapo jambo hilo nalo ni hatari kwani watoto wanakuwa hawana mwangalizi.
Serikali ingeweza kupunguza baadhi ya kero na matatizo kwa wazazi endapo barabara itajengwa kwa wao kununua baiskeli ambayo ingewasaidia kwenda Chita sekondari ya kata kisha kurudi Merela baada ya masomo yao ya kutwa na kuepuka hatari za kupata mimba.
“Wazazi wanalazimika kuingia gharama za kuwapangia vyumba wanafunzi Chita ili kuwapunguzia adha ya usafiri kipindi cha masika ambacho huanza march mwisho na kudumu hadi julai kila mwaka kwa kutembea kwenye maji na kupata mitumbwi katika kina kirefu lakini kama barabara ipo ambapo hali hiyo itawaingiza wazazi gharama ya kununua baiskeli tu.”alisema Chogo.
Adha hiyo imesababisha shule ya msingi Merela kupata walimu wachache wanaopenda kazi na moyo safi wa kuwatumikia watanzania ambao wamekubali kufanya kazi katika mazingira yoyote yale na kuwa kuna wasi wasi umetanda yakukosa waganga wa zahanati ya kijiji cha Merela pindi itapomalizika kutokana na hali halisi ya usafiri ilivyo.
Chogo alitaja neema zinazopatikana katika ukanda wa kijiji hicho kuwa ni kilimo cha mazao aina mbalimbali yakiwemo yale ya ufuta, mpunga, mahindi, mtama, viazi na mihogo huku kukiwa na vitoweo kedekede kutokana na kujaliwa na mito na mabonde yenye rutuba na ufugaji wa wanyama.
MZEE CHOGO AMESIKITISHWA NA DHARAU DHIDI YA AHADI YAWAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YA UJENZI WA BARABARA YACHITA-MERELA.
Mwaka 2005 tasaf ilitoa kiasi cha sh30 mil kwa ajili ya ujenzi wa barabara ikiwemo kuweka matuta. Maravati na madaraja lakini ujenzi huo esa zake zililiwa na wajanja wachache.
Mwaka 2009 Waziri Mizengi Kayanda Pinda alitembelea kijiji cha Merela na lengo kuu ni kusikiliza kero za wananchi ambapo alifanya mkutano kando yadaraja la mto kihansi oktoba 17 mwaka huo.
Kero kuu iliyowasilishwa kwake ni ile ya wajawazito kujifungua vichanga katikamitumbwi tena katikati ya maji, kufariki dunia wakiwa katika machela, na wagonjwa kushindwa kupata tiba kwa wakati muafaka na ile ya kurudisha maitikatika makazi yao kwa ajili ya kuzika.
Sehemu ya mazungumzo hayo yalikuwa hivi ni baada ya waziri kuu kupata kero aina mbalimbali hasa ile ya barabara ambayo ilionekana ni mzigo mkubwa kwa halmashauri kuijenga na kuiagiza wakala wa barabara mkoa (Tanroad) kuchukua jukumu la kuitengeneza hapa ndipo Pinda alipopuuzwa agizo lake na hizi idara kwa sababu wanazozijua wao.
Halmashauri iliulizwa hivi na Pinda.
Mna mpango gani nah ii barabara ya Chita-Merela ?. Na Mkurugenzi wahalmashauri ya Kilombero, alijibu kuwa halmashauri imetenga kiasi cha sh60 milkatika bajeti yake ya fedha ya mwaka 2009/2010 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo wakati wilaya ikiwa chini ya mkuu wa wilaya ya Kilombwro Mhandisi Evalistin Ndikilo ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Pinda: Sh60 Mil na oktoba hii je mmempata mkandarasi ?.
Pinda aliieleza halmashauri kuwa kiasi cha bajeti cha sh60 Mil ni za kupoteza fedha kama hali ndiyo hii mwezi huo wa kumi ?.
Aliuza tena swali lingine kama mwezi wa kumi hali ndiyo hiyo je mwezi wakumi na moja itakuwa je ?.
PINDA ATOA AGIZO KWA TANROAD MKOA.
Katika agizo lake mbele ya mkuu wa mkoa wa Morogoro wakati huo Meja Jeneral Mastaafu, Said Kalembo, mbunge wa jimbo la Kilombero, viongozi waserikali ya wilaya Kilombero na Meneja wa wakala wa barabara wa mkoa waMorogoro (Tanroad) na viongozi wengine Waziri mkuu Mizengo Pinda alitoa agizo hili.
“Waziri mkuu alitoa agizo kuwa pakuwa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwa namna moja ama nyingine haitaweza kuitengeneza barabara ya Chita-Merela badala yake wakala wa barabara mkoa wa Morogoro yenyewe ndiyo itawajibika kuichukua na kuijenga ili wananchi hao waweze kuepukana na adha wanazozipata lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea zaidi ya serikali ile yawilaya na mkoa imeshindwa kutatua kero ya barabara toka 2009 mpaka sasa 2014.”alisema Chogo.
Chogo alielendelea kutoa ufafanuzi kuwa kwa namna anavyofahamu yeye hasa kwa mfumo wa utendaji wa serikali alijua kwa mwaka wa fedha wa mwaka 2010/2011 barabara hiyo ingekuwa tayari imetengewa fedha na halmashauri yenyewe na tanroad ili barabara hiyo kuweza kujengwa lakini ameshangazwa na ukimya uliotanda mpaka sasa.
Alihoji inakuwaje mpaka agizo la waziri kuu halijatekelezwa na kuupuzwa ngaziya mkoa na ile ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero ?.
WAAMIA KWENDA KWA PINDA KUMWELEZA AGIZO LAKO LA UTENGENEZAJI WA BARABARA LIMEPUUZWA.
Sehemu ya wazee wa kijiji cha Merela wameadhimia kwenda jijini Dar es Salaam kuonana na waziri mkuu ili kumweleza kero ya wananchi wa kijiji hicho inavyoendelea na kumkumbusha kuwa agizo lake alitoa kuwaagiza tanroad watengeneza barabara ya Merela-Chita halijatekelezwa na limepuuzwa na viongozi wa ngazi zote mbili za halmashauri ya wilaya na mkoa.
Tulianza mchakato kwa kukaa vikao vya wazee pekee juu ya suala la kwenda kuonana na waziri mkuu kutokana na agizo lake kwa tanroad lakini tukashirikisha watalaam ambayo wengi wao ni vijana na kuunga mkono ambao nao kutushauri kuonana na serikali ya kijiji kisha diwani wetu Hssan Kidapa.alisema Chogo.
Kamati imendwa ya watu tisa itajumuisha wazee, vijana na kuongozwa na diwani wao ambaye ni Mwenyekiti katika kamati hiyo ambayo wananchi na wafanyabiashara wanalazimka kuchangia kiasi cha sh2.5 mili kughalamia safari hiyo kwenda na kurudi.
Mwanana Salum Choma (49) yeye ni mkunga katika kijiji cha Merela alisema kuwa huwajibika kumsindika mama mjazito kutoka Merela kwenda katikazahanati ya Chita na kutoa ushuhuda wengi wanaozalia njiani katika mitumbwi ni wale akinamama wajawazito ambao hajui kusoma tarehe za makisio yakujifungua.
Choma alisema amekuwa akiwazalisha wajawazito nyumbani kwake lakini anapoangalia kadi ya mahudhirio ya klinikini anakuta tayari siku zimepita za makadio ya kujifungua ama imebakia siku moja au mbili.
“Ni kweli wengi wa wajawazito hujifungulia njiani tena katika mitumbwi wakati wakitoka Merela kwenda zahanati ya Chita kufuata huduma za kiafya lakini ni wale waliofuatilia kadi ya maendeleo ya kliniki au wasiojua kusoma na wengi wao nawazalisha hapa hapa nyumbani kwangu.”alisema Choma.
Alisema kuwa hana idadi kamili ya akina mama anaowazalisha nyumbani kwake lakini kwa mwaka 2013 alifanikiwa kuwazalisha akinamama wajawazito 52 wakati kwa mwaka 2013 akizalisha akinamama 25 huku akikokotoa hesabu hiyo kwa wale walioshindikana kuzalishwa kwake kwa mwaka 2013 wakiwa saba wakati akiwasindikiza zahanati ya Chita baada ya yeye kushindwa kutokana na njia ya uzazi kulewa kufunga.Alisema.
Mganga kiongozi wa zahanati ya Chita anadhibitisha wajawazito kujifunguanjia na wagonjwa kupoteza maisha.
Dustan Mkotte ni mganga kiongozi zahanati ya Chita alisema kuna shida yahuduma ya afya kwa wananchi wa Chita na vitongoji vyake hali inayowapelekea kuwafuata iwe masika au kiangazi ili kutoa chanjo kwa watoto, elimu ya uzazi na kliniki kiujumla.
Wengi hujifungulia njiani na kesi hizo hujitokeza wastani wa akinamama watatu kwa mwezi na tunagundua hilo kwa wale ambao wamezalia wakati tayari wamevuka mto kihansi lakini wale wanaozalia njiani kabla ya kuvuka mto kihansi wengi hugeuza na kurudi nyumbani, tunagundua wakati wa utoaji wachanjo. Alisema Mkotte.
Mkotte alisema kuwa kuna hatari ya akinamama wajawazito kupoteza maisha kujifungulia kwa mkunga kutokana na kutokuwa na utalaam wa ziada kwa kushindwa kutambua dalili hatari za mama mjazito.
Alitaja hatari ambayo inaweza kupelekea mama kupata kifo ndani ya saa 24 baada ya kujifungua kuwa ni kupungukiwa kwa damu inayoweza kutoa wakatiwa kujifungua na kuendelea kutoka na kuwa mkunga hana mbinu zaidi ya kuia isitoke kutokana na kutokuwa na vifaa.
Mtoto naye anaweza kupoteza maisha kutokana na kukosa mashine ya kutoa ushafu katika pua na mdomoni unaosababishwa na kukosa hewa na mtoto kufariki dunia ndani ya dakika moja baada ya kuzaliwa.alisema Mkotte.
Athari anazoweza kupata mkunga ni kupata magonjwa ya maambukizi ukiwemo ukimwi kama hakatakuwa mwangalifu kwa mjamzito anayemzalisha inayochangia na kutoa afya ya mwanamke mjamzito.
Katika zahanati hiyo imekuwa ikihudumia magonjwa ya malaria, kifua, kuharisha, upungufu wa damu, magonjwa ya ngizi, minyoo na magonjwa yanayosabaishwa na kila aina za ajali huku vifo vikijitokeza wastani wa watu wawili kwa mwaka wanaotokana na kupoteza maisha na kuuawawa na mamba.
Mganga huyo alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2000 kabla ya kuhamishwa zahanati hiyo na kuhamishiwa nyingine kulikuwa na idadi ya wajawazitokupoteza maisha kwa mwaka akinamama watatu lakini bila shaka baada ya kutoa elimu hali hiyo itapungua kwani kwa sasa ni 20% tu wanaojifungulia njiani.alisema Mkotte.
Zahanati ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 25 hadi 30 kwa siku wakati zahanati hiyo ya Chita inahudumia wagonjwa 56 hadi 70 kwa siku ambapo vijiji vya Chita na Merela ina jumla ya vitongoji 15 na wakazi 22,000 hivyo kuwepo kwa zahanati ya Merela itasaidia kupunguza idadi hiyo ya watu wanaofuati huduma za afya Chita.
Celelin Ndopwele (45) yeye anajishughulisha zaidi na kilimo na mvuvi katikabonde la kihansi ambapo alianza kazi hiyo akiwa na umri wa miaka 20 na kazi yakuvusha wananchi wa Merela na Chita kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Ndopwele anasema kwa sasa ana miaka mitatu katika kazi ya kuvusha watu naye anaeleza ukweli wa wajawazito kujifungua kwenye mitumbwi.
“Ni kweli wajawazito kujifungua katika mitumbwi na kinachofanyika hapo kwanza baharia ni lazima utie nanga mtumbwi pembeni kwenye kina kidogo chamaji na kama kuna kisha wanaume kutoka katika mtumbwi ule na kwenda umbaliwa mita 50 na kuwaacha akinamama kumsaidia mwenzao kujifunguamtoto.”alisema Ndopwele.
Aliongeza kwa kusema kuwa kama kuna kina kirefu cha maji itawalazimu wanaume kugeuza nyuso zao kwa kuangalia macho kule unakotoka mtumbwi ili kuepusha macho kuangalia kitendo cha mwanamke mjamjazito kujifungua ama anasaidiwa kujifungua mtoto.
Alieleza kuwa kuna adha na kero zinazojitokeza katika safari za kusafirisha abiriakatika bonde hilo kipindi cha masika zikiwemo zile za kupambana na vitumbwi vya wanyama adui namba moja kiboko na mamba ambayo wamekuwa wakifanya vitimbwi mita chache katika maeneo yanayopita mitumbwi.
Kazi ya kusafirisha abiria wananchi hutozwa kwa viwango tofauti ikianzia sh1,000, sh1,500 hadi sh2,000 tangu kwa kuanza kwa msimu wa masika marchi mwisho hadi julai kila mwaka na viwango hivyo tozwa kulingana na umbali wamaji.
Kuna jumla ya mitumbwi 13 inayoegeshwa upande wa Chita na ule wa Merela inayofanya kazi kila siku kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 1 usiku katikamazingira magumu ya kutembea na mwanga hafifu na kuambulia kipato cha sh 10,000 hadi 20,000 kwa siku.
Ndopwele anasema kiwango hicho wanazotozwa abiria wao wakati mungine wapo wanaobwebwa bure na nauli pungufu na kujikuta siku nyingine wakiambaulia sh10,000 au pungufu ya hapo.
Akizungumzia Ndopwele, wanyama wakali wa majini kama mamba na viboko wamekuwa wakiibuka jirabi na mitumbwi na kuzua hofu kwa wasafiri wanaotumia chombo hicho kusafiria na kumlazimu bahari kurudi nyuma mtumbwi ili kupisha wanyama kufanya michezo yao ambayo kwa binadamu huwatia hofu ya kuvamiwa.
Kila mwendesha mtumbwi hulazimika kushusha abiria ili kuwapa abiria kuvukakatika daraja la kihansi wakati yeye na mizigo akikatiza katika mto huo ambako kuna njia mbili.
Njia ya kwanza itakulazimu kushikilia machuma ya daraja hilo ili kuweza kuvuka ama kuvuka kwa njia ya kawaida ya kuvuka kwa kukata maji vingine kuna hatariya mtumbwi kupinduka na kusombwa na maji pamoja na mwenyewe kutokana na aina utaingia kwenye mto huo wenye maji yenye kasi.alisema Ndopwele.
DIWANI WA KATA YA CHITA TARAFA YA MNGETA, HAASSAN KIDAPA.
Anaanza na kueleza faida za kujenga barabara ya Chita-Merela kuwa kata hiyo ya Chita kwa wakulima wake endapo watafundiwa kilimo cha kitalaam mazao yatayopatikana yana uwezo wa kulisha wananchi wa mkoa wa Morogoro.
Kata ya Chita ina vijini nane kikiwemo cha Chita, Makutano, Ching’anda, Lufulu, Udagaji, Merela, Idunda na Masita ikiwa na jumla ya vitongoji 29 huku vijiji vitano vikiwa havina uongozi waserikali ambapo vinatarajia kupata viongozi katika uchaguzi waserikali ya vijiji mwezi septemba mwaka huu.
Vijiji mama ndivyo vyenye uongozi wa vijijini vikiwemo Udagaji, Chita na Merela wakati vijiji vitano vikitarajia kupata uongizi hapo baadaye.
Mazao yanayoliyolimwa ni mpunga, mahindi, migomba, ufuta, mtama na zao jipya la kokoa ambalo kwa sasa lina msimu wakewa tatu na mazao mengine ya chakula na biashara. Alisema Kidapa.
Changamoto inayowakabili wananchi wa Chita-Merela ni ukosefu wa barabara inayoweza kupitika kwa nyakati zote za masika na kiangazi kwani tangu imefunguliwa miaka kabla yamwaka 1930 haijapatiwa huduma ya kuwekwa tuta, madaraja na makaravati ambayo ingewezesha kupitika kwa nyakati zote.
“Mwaka 1930 wamisional walijenga daraja la miti na wananchi kuweza kulitumia kwa shughuli mbalimbali lakini kwa kipindi cha kiangazi tu kwani masika ni lazima upande mtumbwi ukuvushe.”alisema Kidapa.
Kidapa alisema kuwa barabara ya Merela-Chita una umbali wakilometa 10.3 kati ya hizo 85% ni kutumia maji na 15% ni sehemu ya nchikavu na mvua kadiri inavyojesha na kutiririshamaji katika bonde la kihansi 15% za nchikavu zinaweza kupungua kutokana na uwingi wa maji.
GHALAMA.
Kwa mujibu wa watalaam kutoka ofisi ya mhandisi halmashauriya wilaya ya Kilombero kufanya tathimini ikinifu na kupata kiasi kisichopungua ya sh2 bilioni kwa ajili ya uwekaji wa vifusi, karavari ndogo za line na zile za boksi na zitawezesha barabara hiyo kupitika kipindi chote cha mwaka.alisema Kidapa.
Kazi ya upembuzi yakinifu ya mwaka 2012-2013 chini yamhandisi Mbena wa halmashauri hiyo ilifanya kazi hiyo.
KWANI NINI DIWANI ANAIFUATILIA BARABARA HIYOYA MERELA-CHITA ?.
Kidapa alisema moja ya sababu ya kuifuatilia barabara hiyo ili ijengwe na serikali ni baada ya karibu ya kero za msingi katikakata yake kupungua kwa 65% hasa zile za kijamii.
Alitaja kero zilizofanikiwa kutatuliwa kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, serikali ya kata na halmashauri ya wilaya yaKilombero kuwa ni ujenzi wa soko jipya la kata hiyo, Kituo kikuu cha polisi, wodi ya wazazi, nyumba za waganga na ofisi ya kijiji cha Chita.
Alifafanua kuwa kituo cha polisi kwa sasa imebakia hatua yakuweka milango, madirisha na thamani za ndani na kituo hicho kinatakapomalizika kitakuwa kituo chenye kuhidhi mahitaji muhimu ya ikitarajia kighalimu kiasi cha zaidi yash47.4mil.alisema Kidapa.
Soko limekamilika kwa ujenzi wake ikighalimu kiasi cha sh55 mil zikitolewa na halmashauri ya wilaya Kilombero, daraja la muda la mto Mlumbaji lenyewe likitumia sh11.9 mil linalotumiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Chita. Alisema Kidapa.
Wodi ya watoto, akinamama wajawazito imetumika sh110 kutoka halmashauri hiyo na ofisi ya kijiji na kata ambapo sh13 zimetumika.
Baada ya kuingia madarakani nilikuwa naifahamu hii kero yaukosefu wa barabara kwa wakazi wa Merela na Chita na nilichofanya niliwasilisha hoja katika kikao cha pili cha baraza la madiwani kwa halmashauri.alisema Kidapa.
Jibu lililotolewa na halmashauri kuwa haina uwezo wakuitengeneza barabara hiyo ya Chita-Merela na kujulishwa kuwa wakala wa barabara mkoa ndiyo wenye jukumu la kuitengeneza kwa agizo la waziri mkuu Mizengo Kayanda Pinda mwaka 2009.
Kutokana na kumbukumbu zilizopo zinabainisha tanroad ilikataa agizo hilo la kutengeneza barabara hiyo kwa kueleza kuwa haina vigezo lakini halmashauri inadaiwa baada ya agizo hilo haikuweza kuifuatilia kwa wakala wa barabara mkoa kuona ishikilia kidete na kutengezwa kwa barabara.
Alisema Baada ya kuingia madarakani nilikuwa naifahamu keroya barabara kwa wakazi wa Merela na Chita na nilichofanya niliwasilisha hoja ya Kidapa.
HALMASHAURI YASAKA WADAU WA KUTENGENEZA BARABARA.
Halmashauri ilianza kutafuta wadau wengine na kupata USAIDya Marekani ambayo imekubali kusaidia kuitengeneza barabaraya Chita-Merela lakini ni baada ya vigezo walivyoomba kuviridhia.
Moja ya vigezo vilivyowekwa na USAID ni pamoja kutaka kujua watumiaji wa vyombo vya usafiri, idadi ya watu wanaotembea kwa miguu kwa siki, uwepo wa shule na huduma za afya, uchumi na uwekezaji ambavyo kimsingi barabara hiyo imekithi na kufaulu. Alisema Diwani huyo.
Diwani huyo alisema kuwa wakati wa masika hakuna chombo chochote kinachotumika katika barabara hiyo zaidi ya kutembea kwa miguu na kama utabeba baiskeli itakusaidia kukokota katikaumbali huo wa kilometa 10.3 kwa kutumia muda wa saa 3 na kusaidia kama umefunga mzigo ambayo utaona kero kuubeba kichwani.
“Shida bado ipo tena kwa kiasi kikubwa na endapo serikali au wadau wengine wa serikali watajenga hiyo barabara, wananchi wataepukana na kero ya kutembea katika maji saa 1:30, nchikavu 15 na katika mtumbwi muda wa saa 1 hii ndiyo hali halisi ya masika.”alisema Kidapa.
Katika uchambuzi yakinifu ya barabara hiyo ambayo inatarajiwa kutumika cha sh2. Bil imebainika ni kilometa nne ndizo zitahitajika kuweka karavati, madaraja na sehemu kuwekwa tuta ili kuzuia maji na kuelekeza kwenda mtoni na sehemu yabarabara kuwa salama na watu kupita kwa nyakati zote. Alisema diwani huyo.
DIWANI AWATUPIA LAWAMA HALMASHAURI YAWILAYA KILOMBERO.
Kidapa alisema kuwa halmashauri inawajibika kwa lawama zote juu ya kutojengwa daraja hilo katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu baada ya waziri mkuu kutoa agizo la kuwataka tanroad kuchukua jukumu la kujenga barabara kuwa hakukuwa na ufuatiliaji wa dhati wa tanroad ambao ungetoa msukumo wakujengwa barabara.
Ndiyo maana wazee wa kijiji cha Merela wameona ni bora kufunga safari ya kwenda kwa waziri mkuu kumweleza kuwa lile agizo lake halitekelezwa na tanroad la kujenga barabara yaMerela-Chita lakini hata halmashauri nao hawakutoa msukumo wowotw kwa tanroad.alisema Kidapa.
“Kwanini wazee wetu wamechukua jukumu la kwenda kwa waziri mkuu ?, jibu ni lahisi tu ni kwamba wamechoka na hii kero ya kutembea kwenye maji na wajawazito kujifungulia njiani tena katika mitumbwi na wagonjwa kufariki dunia wakifuata huduma za afya Chita inakera lakini tutapambana na bila shaka serikali itasikia kilio chetu na siku ya siku barabara itajengwa.” Alisema Kidapa.
MKUU WA WILAYA YA KILOMBERO AELEZA NAMNA WALIVYOVALIA NJUGA BARABARA YA MERELA-CHITA.
Serikali ya wilaya kwa mwaka wa fedha 20134/2014 imetenga kiasi cha sh47 mil kwa ajili ya barabara ya Chita-Merela fedha ambazo zitatumika kuanza kutengeneza vipande kwa vipande. Alisema Hassan Massala ambaye ni mkuu wa wilaya yaKilombero.
Massala alisema kuwa barabara ya Chita-Merela imechukuliwa na wakala wa barabara mkoa wao ndiyo wanawajibika kuitengeneza na halmashauri inajaribu kutenga kiasi cha fedha mwaka hadi mwaka ili kusaidia kuitengeneza kwa awamu na halmashauri ipo katika mchakato wa kuifuatilia agizo la waziri mkuu kwa tanroad kuona wanatekeleza agizo lake.
“Hii barabara kweli ina kero na ina changamoto nyingine kwa wakazi wa Merela hata wale wa Chita, mimi mwenyewe decemba 2013 nilifika kijiji cha Merela lakini kwa usafiri wa treka kwani wakati huo maji yalikuwa kidogo katika harakati za kusuluhisha migogoro ya wakulima na wafugaji.”alisema Massala.
TANROAD MKOA MOROGORO WANAJESEMA JUU YAKUJENGA BARABARA HIYO YA MERELA-CHITA ?.
Meneja wa wakala wa mkoa wa Morogoro (Tanroad) Doroth Mtenga anaeleza kuwa barabara ya Chita-Merela kwa sasa haina sifa ya wao kama wakala kuichukua na kuijenga mpanga ipandishwe hadhi ya mkoa.
Mtenga alisema kuwa kinachofanyika kwa sasa juu ya barabara hiyo ni kuipandisha hadhi kutoka ile ya halmashauri hadi mkoa na mchakato huo una utaratibu wake na kama itapandishwa hadhi hakutakuwa na kipingamizi kutokana na vigezo vilivyopo vya kiuchumi.
“Ni kweli wakazi wa Merela wana uhitaji wa barabara na hii barabara ya Chita hadi Merela ina umbali wa kilombeta 10, tanroad itaitengeneza mara baada ya kupandishwa hadhi kutoka ile ya halmashauri hadi mkoa ndiyo sisi tunakuwa na haki yakuiingiza katika mipango yetu lakini kwa sasa ipo katikamchakato wa kuipandisha daraja letu.”alisema Mtenga.
Aliongeza kwa kusema barabara ya Chita-Merela kwa sasa ipokatika mpango wa orodha ya barabara za wilaya Kilombero zilizopendekezwa kupandishwa daraja kuwa ya mkoa katikaorodha iliyopitishwa na bodi ya barabara mkoa wa Morogoro.
Mtenga alisema kuwa kwa sasa wananchi wanapaswa kusuburi kwa muda mfupi kwani mipango ya kuwakomboa ipo mbioni na kuchelewa kwake kumetokana na mfumo mzima wa kuipandisha daraja ili iwe na sifa ya wakala wa barabara kuitengeneza kwani subira yavuta heri.CHANZO:MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment