BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANARIADHA WA AFRIKA YA KUSINI OSCAR PISTORIUS APATIKANA NA HATIA KUMUUA MPENZI WAKE, AFUNGWA MIAKA MITANO JELA.

Olympic and Paralympic track star Oscar Pistorius sits in the dock at the North Gauteng High Court in Pretoria March 11, 2014. Pistorius is on trial for the murder of his girlfriend Reeva Steenkamp at his suburban Pretoria home on Valentine's Day last year. REUTERS/Kim Ludbrook/Pool  (SOUTH AFRICA - Tags: SPORT CRIME LAW)
Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia.
 
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.


 
Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.

Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.

Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: