BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SITTA ABASI MTEMVU NI MISS TANZANIA 2014 HAKUDANGANYA UMRI.


Mshindi wa Miss Tanzania Sitti Mtemvu"katikati" pamoja na warembo wengine, kulia kwake ni mshindi wa pili Jihhan Dimachk na kushoto kwake ni Lilian Kamazima mshindi wa tatu. 


Ushindi wa Bi Sitti Abbas Mtemvu katika kinyang'anyiro cha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania ya mwaka 2014 umezua shutuma juu ya uhalali wa mrembo huyo kuvikwa taji hilo.


Siku chache baada ya kutangazwa kwake kuliibuka shutuma mbalimbali dhidi ya Bi Sitti na kumwondolea vigezo vya umalkia huo wa urembo.Tuhuma hizo zilianza kuzagaa katika mitandao ya habari ya kijamii zikiwemo shutuma za kufanyika udanganyifu wa umri.

Kamati ya kuandaa mashindano hayo, siku ya Jumanne imelitolea ufafanuzi suala hilo,mjini Dar es Salaam, ambapo mkurugenzi mtendaji wa kamati hiyo, Hashim Lundenga amesema, Sitti ndiye mshindi halali wa mashindano hayo ya mwaka 2014, na kwamba shutuma dhidi yake hazina msingi wowote zaidi ya kuwa uzushi: 


"Mimi nasema shutuma zote zilizotolewa hapa ni shutuma za uongo, kwa sababu kulingana na taratibu nilizozieleza hapo awali, sisi kama kamati kama waandaaji wa Miss Tanzania hatuna matatizo yoyote" anasema Bwana Lundenga.

Akizungumzia tuhuma kwamba Bi Sitti alidanganya umri kuwa ana miaka 18, mkurugenzi mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania, Bwana Lundenga ameshangazwa na uzushi huo, akisema mrembo huyo hajawahi kutaja umri huo kama ndio umri wake. "hakuna mahala popote alipozungumza kuwa ana miaka 18...Kwa hiyo ni rumours ambazo zinaendelea tu na wameshindwa kuhakikisha"

Kwa ufafanuzi wa waandaaji wa mashindano hayo, Sitti Abbas Mtemvu ni mshindi halali wa Miss Tanzania 2014 na ndiye anayetarajiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya mrembo wa dunia ya Miss World yatakayofanyika 2015.BBC

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: