Kikao cha Bunge la Tanzania kilichoahirishwa siku ya jana Novemba 29 ni moja ya vikao ambavyo vilivuta hisia za watu wengi na kutengeneza historia nyingine mpya kutokana na mjadala wa ishu ya Escrow, baada ya kikao hicho kuahirishwa Wabunge Ezekiel Maige, Aeshi Hilary, David Kafulila na Mchungaji Peter Msigwa walizungumzia kuhusu maamuzi ya Bunge hilo.
“Tumekuwa na Bunge la kipekee sana katika muda wangu wa kuwa Mbunge karibu miaka nane sasa, hii ni experience yangu ya kwanza kuwa na kipindi kigumu kama hiki. Bunge limekuwa kwenye mtihani wa ama kuamua kulinda viwango vyake vya utendaji wa miaka yote au kuamua kuwa na viwango tofauti…” —Ezekiel Maige.
“… Niwaombe Watanzania wawe wavumilivu kila kitu kina wakati wake na muda wake… Nilipongeze Bunge, nipongeze kamati ya usuluhishi vilevile nimpongeze Waziri Mkuu kwa kukubaliana na haya, ninaamini Serikali itachukua hatua zake…”– Aeshi Hilary.
“…Niliamini siku zote kwamba kuna makosa yamefanyika katika utoaji wa fedha zile na chunguzi za CAG, PCCB, na hatimaye kamati ya PAC zimeonyesha hivyo na hatimaye Bunge limeweza kuchukua hatua hii. Kuna changamoto nyingi katika kupambana na mambo kama haya, kuna vitisho, kudhalilishwa mimi niliitwa ‘tumbili’ na kuna watu walitishia kuniua, lakini yote kwa ujumla wake ni changamoto katika kupambania yale ninayoamini…” –David Kafulila.
“… Tumetimiza wajibu wetu kuishauri Serikali, tumeona watu wengine hawakutimiza wajibu wao… Upande wetu wa upinzani tuling’ang’ania kwamba watu wawajibike, niwasihi wananchi tuendelee kushirikiana kwa sababu mwisho wa siku hii ni nyumba ya kwetu sote mtu yeyote asiyetimiza wajibu wake lazima abebe mzigo wake …”—Mchungaji Peter Msigwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ KAFULILA, MSIGWA WATAKUWA WANAONGOZWA KUCHUKIWA NA PROFESA MUHONGO NA TIBAIJUKA TU !!!.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment