TASWIYA MATUKIO AJALI YA HELKOPTA YA MALIASI NA UTALII ILIYOUA RUBANI WANNE NDIYO HAYA JIJINI DAR ES SALAAM..
Helkopta aina ya Chopa iliyoanguka maeneo ya Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi na kuua watu wanne waliokuwemo rubani pamoja na askari watatu.
Miili ya watu waliokuwemo kwenye helkopta hiyo ikiwa imekandamizwa na mabaki ya chopa hiyo.
Sehemu ya mashuhuda wa maeneo hayo wakishuhudia ajali hiyo.
Helikopta inayosemekana inamilikiwa na TANAPA imeanguka na kuteketea kwa moto katika eneo la Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema waliona helkopta hiyo ikipoteza uelekeo na badaye kuanguka chini hali iliyosababisha kishindo kikubwa baada ya kulipuka moto.
Inasemekana ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu wanne ambao wote wameripotiwa kufariki dunia. Aidha imeelezwa kuwa katika ajali hiyo kulikuwamo na Askari 3 na rubani. http://www.sufianimafoto.com
0 comments:
Post a Comment