BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA SASA SIYO DILI TENA TANZANIA.
Kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya nchini kimesema kitazidisha nguvu katika kupambana kuwadhibiti wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo, waingizaji na watumiaji.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa, wakati akihojiwa na kuhusu mikakatika ya kikosi chake ya kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya na watumiaji.
Alisema wamegundua mbinu ambazo zinatumiwa na wafanya biashara wa dawa hizo kuziingiza nchini na kwamba kikosi chake kimejipanga kikamilifu kukabiliana nao.
Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa.
“Tumejipanga vizuri kwenye mipaka yote, baharini hata kwa wale wanaotumia magari kusafirishia dawa hizo kwani hivi sasa wafanyabiashara hawa wamekuja na mbinu nyingi kama za kuficha madawa hayo kwenye mabomba ya gesi, simtank, samaki wabichi huku wengine wakibeba kwenye mikasi ya kukatia michongoma,” alisema Nzowa.
Alisema dawa zinazoingizwa nchini kwa wingi nchini ni Cocain na Heroin na njia wanazotumia ni bahari na kulifanya Jiji la Dar es Saalam kuongoza kwa uingizaji wa dawa hizo likifuatiwa na Tanga kisha Lindi.
Kutokana na malalamiko ya watu wengi wakidai kuwa wanaokamatwa ni watumiaji tu huku wakiwaacha wafanyabiasha wanaowatuma, Nzowa alisema hakuna atakayesalimika kwani hadi sasa wamekamata robo tatu ya wafanyabiashara wakubwa na kesi zao zipo mahakamani. CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment