BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

COASTAL UNION YAIPIGIA HESABU KALI NDANDA FC MTWARA.

https://pamelamollel.files.wordpress.com/2012/10/dscf1663.jpgTIMU ya Coastal Union ya Tanga imeondoka mkoani hapa leo asubuhi kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda SC itakayochezwa
Jumamosi wiki hii.

Coastal Union ambayo mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City iliyochezwa kwenye uwanja wa
CCM Mkwakwani haikupata matokeo mazuri sana baada ya kulazimishwa sare hivo itaingia kwenye mechi hiyo mithili ya mbogo aliyejeruhiwa msituni

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Mkenya
James Nandwa alisema kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi baada ya kuyafanyia kazi kwa
asilimia kubwa mapungufu yaliyojitokeza mechi iliyopita.

Alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha kikosi hicho kinaibuka na ushindi kwenye
mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu msimu huu
kuonekana kujiimarisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

"Kikosi changu kipo imara kuweza kuwakabili Ndanda SC ikiwemo kuhakikisha tunapata
matokeo mazuri hii inatokana na maandalizi kabambe tuliyoyafanya hasa kubwa kurekebisha
baadhi ya maeneo kwenye kikosi hiki "Alisema Kocha Nandwa.

Alisema kuwa mipango yake hivi sasa ni kukiwezesha kikosi cha timu hiyo kuweza kufanya
vizuri kwenye mechi zao zijazo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa
Ligi kuu hapa nchini.

Msafara wa Coastal Union uliondoka leo mkoani hapa kuelekea mkoani Mtwara unaongozwa
na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ,Albert Peter ambapo baada ya kuwasili mkoani mtwara
utafanya mazoezi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: