FBI WAKAMATA WATU WATATU KWA NJAMA ZA KUMUA RAIS BARACK OBAMA, WANASWA UWANJA WA NDEGE.
Maafisa wa Marekani wamewakamata wanaume watatu Jumatano kwa tuhuma za kupanga njama za kuunga mkono kundi la kigaidi la Islamic State nchini Syria na kumwua rais Barack Obama, polisi na mawakala wa idara ya makosa ya jinai ya Marekani (FBI) ndani ya Marekani.
Maafisa wanasema wanaume wote watatu walikuwa wakiishi jijini New York ingawa wawili wametambulishwa kama raia wa Uzbekistan na wa tatu kama raia wa Kazakhstan.
Wizara ya sheria ya Marekani inasema maafisa waliwakamata Akhror Saidakhmetov raia wa Kazakhstan katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy ,New York akijaribu kuingia ndege ya Uturuki kuelekea Syria.
Maafisa hao walisema raia wa Uzbekistan Abdurasul Hasanovich Juraboev, alinunua tikiti ya ndege ya kutoka New York kuelekea Istanbul na alikuwa amepanga kuondoka Marekani mwezi ujao.
Wanasema mtuhumiwa wa pili kutoka Uzbekistan Abror Habibov, alimpa msaada wa kifedha mwenzake Saidakhmetov kujiunga na kundi la Islamic State.
Wizara ya sheria ya Marekani inasema Juraboeve alikuwa tayari kufanya shambulizi la kigaidi ndani ya Marekani endapo kundi la Islamic State lingemtaka afanye hivyo.
Kamishina wa polisi jijini New York William Bratton aliwaambia wandishi habari kuwa “hii ni hali halisi.”
Alisema kwamba huu ndiyo wasiwasi mkubwa uliopo kwamba watu binafsi wanachochewa bila kuwahi kwenda Mashariki ya Kati, au kwenda Mashariki ya Katin kupata mafunzo ya kupigana na kisha kutafuta njia za kurejea nchini. http://www.voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment