BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KESI YA SHEIKHE PONDA KUSIKILIZWA LEO, SHAHIDI WA TATU KUTOA USHAIHIDI MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOROGORO.

Picha ya maktaba Mtanda Blog akiopnekana Sheikhe Ponda Issa Ponda mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.

Hamida Shariff, Morogoro.
Kesi inayomkabili kiongozi wa Jumuiya na taasisi za kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro inaendelea kusikilizwa kesho Februari 2 ambapo shahidi wa tatu atatoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Kesi hiyo yenye mashahidi 15 wa upande wa mashtaka ilianza kusikilizwa Januari 26 mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Mary Moyo.



Katika kesi hiyo Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali ya Mahakama, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo yote hayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka 2013 katika uwanja wa Shule ya msingi Kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro.

Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ni aliyekuwa mkuu wa polisi Wilaya ya Morogoro (OCD) Sadick Tindwa ambaye kwa sasa ni mkuu wa polisi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga na shahidi wa pili ni aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro (RCO) Jafert Kibona ambaye kwa sasa ni Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mtwara.

Pamoja na mashahidi hao Wakili wa upande wa Serikali Benard Kongola aliieleza mahakama kuwa vipo vielelezo vitakavyotolewa mahakamani hapo ambapo mpaka sasa tayari kimeshatolewa kielelezo kimoja ambacho ni kibali cha kuruhusu kufanyika kwa kongamano la Eid pili ya mwaka 2013 ambacho kilicholewa na shahidi wa kwanza.

Wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa Sheikh Ponda bado yuko rumande kutokana na mahakama hiyo kushindwa kumpa dhamana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na hati iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP ya kuzuia dhamana ya mshtakiwa huyo kwa maslahi ya Taifa.

Mawakili wanaomtetea Sheikh Ponda ni Juma Nasoro, Bathoromeo Tarimo na Abubakar Salim wakati upande wa mashtaka unaongozwa na wakili mkuu mwandamizi wa Serikali kanda ya Mshariki Benard Kongola, Sunday Hyra na George Mbalasa.

Kesi hiyo yenye mvuto kwa watu wengi wa mkoani Morogoro wakiwemo wafuasi wa Sheikh Ponda imekuwa ikiendeshwa huku ulinzi mkali wa polisi wenye silaha za moto, mabomu ya machozi ukiwa umeimarishwa katika viunga vya mahakama hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: