LIVE MARCH: DK 90: YANGA YAIBOMOA KLABU YA BDF XI YA BOTSWANA KWA BAO 2-0, HAMIS TAMWE NDIYE SHUJAA.
Winga wa klabu ya Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa bao 2 - 0. Winga machachari wa Yanga, Saimon Msuva kushoto akipiga hesabu za kumpita beki wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana, Othusitse Mpharitlhe wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam. Bao hizo zimepachikwa wavuni na mshambuliaji Amis Tamwe katika mchezo huo. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
0 comments:
Post a Comment