Bunduki aina ya Submachine gun
Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga.
Tanga. Hali tete na taharuki imezuka katika Jiji la Tanga kuanzia jana baada ya kusikika milio na mabomu na risasi zilizokuwa zikirushwa wakati vikosi vya jeshi la polisi na JWTZ vikishambuliana na kundi linalodaiwa kuwa ni la majambazi.
Milio hiyo imesababisha baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Karasha Amboni Jijini Tanga kulazimika kuhama makazi kusalimisha uhai wao huku askari sita wa jeshi la wananchi (JWTZ) na wa polisi wakidaiwa kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga jana Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja amesema kuwa hiyo ilikuwa ni oparesheni ya ushirikiano wa Polisi na jeshi, JWTZ lengo likiwa ni kudhibiti uhalifu nchini.
“Baada ya askari kufika mapangoni, kundi la majambazi lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano, askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.
Shuhuda mmoja ambaye ni mkazi wa eneo hilo, Rehema Juma (34) amesema yeye na mwenzake walilazimika kuhama kwenye nyumba zao kukimbia mapigano hayo kwa kuhofia maisha yao
“Kilichosababisha tuhame ni milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona helikopta ikirandaranda tukapata hofu kubwa... hatuwezi tena kutoka kwenye nyumba zetu,” amesema Rehema Juma ambaye yeye na watoto wake watatu wamelazimika kuhifadhiwa kwa ndugu zake mtaa wa Amboni.MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MAJAMBAZI WAWAHENYESHA ASKARI WA JWTZ NA JESHI LA POLISI KATIKA JIJI LA TANGA MAPANGO YA AMBONI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment