MATUMIZI YA UVUTAJI WA BANGI SASA RUKSA.
MJI wa Washington DC wa Marekani umehalalisha matumizi wa bangi mjini hapo.
Hatua hiyo ya mji wa Washington kuhalalisha matumizi ya bangi inafuatia baada ya ile ya jimbo la Colorado, Alaska na Washington State kuhalalisha matumizi ya mihadarati kwa starehe.
Mpango huo umekubalika na wananchi wengi katika kura ya maoni iliyopigwa mjini hapo Novemba mwaka jana.
Kulingana na sheria hiyo wale waliokuwa wakimiliki bangi kisiri watakuwa huru kuivuta bila hofu ya kukamatwa.
Mpaka sasa sheria hiyo mpya imezua tofauti baina ya Meya wa mji huo na bunge la Congress.
Kulingana na sheria hiyo wenyeji wa mji huo wenye umri unaozidi miaka 21 watakuwa huru kumiliki gramu 56 ya Bangi.
Pia sheria hiyo imeidhinisha kuwa raia wanaruhusa ya kupanda bangi majumbani mwao.
Kwa mujibu wa BBC, mji wa Washington DC - ni wilaya maalum lakini haina uhuru na hadhi sawa na majimbo kwa hivyo kuna dhana kuwa ilikiuka kanuni ilipoamua kupiga kura ya maoni.
Katika barua iliyoandikwa na wajumbe wa bunge hilo la Congress, Meya wa Washington Muriel Bowser ameonywa kuwa sheria za jimbo zinakiukwa iwapo sheria hiyo maarufu itaanza kutekelezwa.
Wajumbe hao wanadai kuwa kulingana na sheria maalum iliyopitishwa na bajeti la taifa Kuhalalishwa kwa bangi ni haramu.
Hata hivyo meya wa Washington DC ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa walifuata kanuni zote zilizowekwa katika kuhalalisha utumiaji wa bangi mjini hapo.MAJIRA.
0 comments:
Post a Comment