Rubani akishuka na kifaa maalumu kutoka kwenye ndege wakati ikiwa angani, kifaa hicho hutumika wakati ndege imepatwa na hitilafu na kuhatarisha usalama.
Baadhi ya wanajeshi wakiangalia mabaki ya ndege ya kivita iliyoanguka katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza jana. PICHA: KWA HISANI YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA.
Rubani wa ndege ya kivita ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Meja Peter Lyamunda, amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akiitumia kuteketea katika uwanja wa Ndege wa kivita mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa JWTZ Makao Makuu Dar es Salaam, Meja Joseph Masanja, alisema ajali hiyo imetokea jana mchana wakati ndege hiyo ikiwa katika hatua za mwisho za kuruka hewani.
Alifafanua kuwa wakati ndegevita zikiwa katika mazoezi yake ya kawaida, ndege (mnyama) aliingia katika injini ya ndege hiyo na kuisababishia kuwaka moto.
Moja ya ndege za kivita ikiwa angani.
“ Meja Lyamunda, alipogundua ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje kwa kutumia vifaa maalumu vya kujiokoa, ingawa amepatwa na majeraha hasa katika mguu wake lakini kwa sasa hali yake ni nzuri na anaendelea na matibabu,”alisema Meja Masanja.
Kutokana na ajali hiyo aliwaondoa hofu wananchi hususani wanaofanya shughuli zao jirani na viwanja hivyo kuendelea na shughuli zao za kila siku. CHANZO: NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ NDEGE MNYAMA ASABABISHA NDEGE YA KIVITA YA JWTZ KUPATA AJALI NA KUWAKA MOTO, RUBANI ATUMBIA MBINU ZA KIJESHI KUJIOKO AKIWA ANGANI MWANZA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment