SIMBA SC YAITULIZA POLISI MORO SC UWANJA WA JAMHURI, LIGI KUU TANZANIA BARA.
Klabu ya Simba SC imeituliza Polisi Moro SC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika uwanja wa jamhuri Morogoro kwa Simba kupata ushindi wa bao 2-0.
Mshambuliaji Ibrahim Atib alipachika bao la kwanza kwa klabu yake kwa kichwa akitumia uzembe wa mabeki wa Polisi Moro SC walioshindwa kucheza mpira wa kurushwa na mpira kujaa wavuni wakati bao la pili lilifungwa na mshambuliaji Elias Maguli aliyetumia pia uzembe wa mabeki na kipa kuruhusu mpira kuwapita kizembe.
0 comments:
Post a Comment