Kocha Mohamed Adolph RishardNa Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Polisi Morogoro SC imekatisha mkataba na kocha wake mkuu wa klabu hiyo, Mohamed Adolph Rishard kutokana na timu hiyo kucheza chini ya kiwango na kusababisha timu kushika nafasi za chini za msimamo wa ligi kuu Tanzania bara mkoani hapa.
Akizungumza na Mtanda Blog mjini hapa, Mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro SC, Zuberi Chambera alieleza kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Mohamed Adolph Richard amevunjiwa mkataba wake wa kuifundisha timu kutokana na kufanya vibaya huku maamuzi hayo yakifikiwa kwa pamoja na kikao cha kamati tendaji ya timu hiyo kilichofanyika kwenye hoteli ya Top Life jana.
Chembera alisema kuwa kwa sasa timu hiyo itanolewa na kocha msaidizi, John Tamba wakati wakisaka kocha mkuu mwenye sifa za kufundisha ligi kuu Tanzania bara.
“Ni kweli kocha wetu mkuu, Mohamed Adolph Rishard amesimamishwa kufundisha timu yetu kutokana na sababu zilizotolewa na kupitishwa na kamati tendaji ya timu ya kumsimamisha kufundisha na timu ya Polisi Moro SC baada ya kucheza chini ya kiwango tofauti na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkataba wetu.”alisema Chembera.
Kikao hicho kimetoa sababu na kuamua kumsimamisha Adolph kutokana na timu kucheza chini ya kiwango kinyume na mkataba wake kwani Polisi Moro SC imepoteza michezo minne, sare nane na kushinda michezo minne ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu katika mzunguko wa kwanza na pili.
Naye kocha wa Polisi Moro SC, Mohamed Rishard akizungumzia kusitishiwa mkataba na klabu ya Polisi Moro SC alisema kuwa suala la yeye kukatishwa mkataba amelipokea kwa mikono miwili kutokana na timu kufanya vibaya.
Richard alisema kuwa mkataba alioingia nao klabu ya Polisi Moro SC ilikuwepo kipengere cha endapo timu itafanya vibaya kwa kupoteza michezo mitatu mfululizo, kamati kuu itamwita na kumhoji kwanini timu imefanya vibaya na kitu hicho kimetokea baada ya timu kufanya vibaya michezo mitatu.
“Ni kweli mkataba wangu wa kuifundisha klabu ya Polisi Moro SC umesitishwa kutokana na timu kufanya vibaya na nimeitwa na kamati tendaji na kuhojiwa kwanini timu inafanya vibaya nami nimejieleza lakini kamati hiyo imefikia uamuzi wa kunisimamisha kazi, nasema sawa nimekubaliana nao”.alisema Adolf.
Adolph aliongeza kwa kusema kuwa wakati wanafikia maamuzi ya kumsimamisha kufundisha Polisi Moro SC yeye alikuwa ameondoka katika kikao hicho baada ya kuhojiwa na kutoa majibu.
“Sawa ndugu mwandishi kama wametangaza kunisimamisha kufundisha Polisi Moro SC, kwani katika mkataba wetu ilikuwemo kipengele cha timu ikifungwa mechi tatu mfululizo nitaitwa na kamati kuu ya klabu ya Polisi Moro SC, sasa ndivyo hali ilivyo kwani tumepoteza michezo mitatu mfululizo kwa kufungwa na Simba SC kwa kufungwa bao 2-0, Kagera Sugar bao 1-0 kabla ya Mtibwa Sugar kuilaza kwa bao 2-1”.alisema Adolph.
Adolph alisema kuwa uongozi wa klabu ya Polisi Moro SC wanahaki ya kuvunja mkataba na yeye na wapo sahihi na yeye amekubali na wala hajaonewa kwani timu imefungwa mechi tatu mfululizo.
“Ligi imebakiwa na mechi nane ili imalizike lakini natoa tahadhari kwa kocha atayeridhi mikoba yangu kujenga falsa iliyo bora ili aivushe timu na janga la kushuka daraja maana isije kama mimi nilivyoikuta timu wakati ina pointi nne na kuambulia pointi 25 aambazo hazikusaidia kukwepa mkasi wa kushuka daraja misimu miwili iliyopita kabla ya kurejea tena ligi kuu Tanzania bara”.alisema Adolph.
Polisi Moro SC kwa sasa ina pointi 20 na anaiombea heri ifanye vizuri katika michezo nane iliyobakia.
Kocha Mohamed Adolph Rishard aliunga na klabu ya Polisi Moro wakati timu hiyo ikiwa ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili msimu wa mwaka 2013/2014 na kushuka daraja kabla ya kurejea tena ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2014.
Katika ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2015 klabu ya Polisi Moro SC imefanikiwa kushinda michezo minne kufungwa michezo minne na sare nne huku zikifungwa na klabu za Simba SC kwa ushindi wa bao 2-0 huku klabu ya Yanga SC, Kagera Sugar FC zenyewe ziibuka na ushindi wa bao 1-0, kabla ya Mtibwa Sugar ikiilaza kwa bao 2-1 huku mchezo wa Ruvu Shooting Stars ikitoa sare tasa ya 0-0.

0 comments:
Post a Comment