BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKALA YA MWANAFUNZI BORA KWA DARASA LA NNE 2014 MKOA WA MOROGORO AIBUKA SHULE YA MSINGI KIWANDANI, MTIBWA SUGAR TURIANI.

 Vaishnavi Vivek Sanil.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mfumo wa malezi bora kwa mtoto sambamba na kumjengea misingi mizuri, ni chanzo kizuri cha mtoto kufanya vizuri katika mambo mbalimbali ikiwemo upande wa elimu.
 
Usemi huo umedhihilisha kwa mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Kiwandani kata ya Mtibwa-Turiani wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Vaishnavi Vivek Sanil kuonyesha dalili za kipaji kikubwa katika upande wa elimu akiwa na miaka 9 tu.

Kipaji cha mwanafunzi, Vaishnavi Vivek Sanil kilianza kuonekana mapema tangu akiwa darasa la kwanza shule ya Kiwandani na kufikia darasa la nne walimu na wanafunzi hawakushangazwa na kipaji chake, kwani alionyesha kipaji katika mtihani wa taifa wa kuingia darasa la tano kwa kushika nafasi ya kwanza kishule, wilaya Mvomero na mkoa.

Katika makala haya mwandishi wa gazeti hili aliongea na mwanafunzi huyo nyumbani kwao Kiwandani-Mtibwa kufichua siri ya mafanikio yake na kushika nafasi ya kwanza kimkoa mtihani wa darasa la nne kuingia la tano.

Vaishnavi Vivek Sanil anaanza kwa kuelezea historia yake fupi kuwa alizaliwa jani 23 mwaka 2006 nchini India na kuanza elimu ya awali katika shule ya msingi Namagunga Girls katika mji wa Lugazi nchini Uganda miaka mitatu kabla ya kuanza shule ya msingi.

Vaishnavi anasema kuwa anawashukuru wazazi wake kwa kumjengea misingi bora na malezi mazuri ambayo yamesababisha yeye kupenda elimu na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mtihani wa taifa wa darasa la nne 2014 katika mkoa wa Morogoro.

“Nimeanza masomo ya darasa la kwanza shule ya msingi Kiwandani mwezi wa tano mwaka 2011, wakati huo wenzangu tayari wamesogea mbele kimasomo na kukabiliwa na changamoto ya lugha ya kiswahili nilikuwa siijui kabisa lakini nilipambana ndani ya miezi miwili nikawa naifahamu kwa kiasi fulani namshukuru mungu, sasa kiswahili nakijua kuongea na kuandika.”alisema Vaishnavi.
Mwanafunzi bora wa mkoa wa Morogoro na wilaya ya Mvomero, Vaishnavi Vivek Sanil (9) akiwa na wazazi wake Vivek Sanil(45) na mama yake Anita Sanil (32) katika picha ya pamoja mara baada ya kufanyiwa hafla ya kumpongeza kwa kushika nafasi hizo katika ukumbi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa kata ya Mtibwa-Turiani Morogoro. Juma Mtanda.
 
Vaishnavi alisema alianza kusoma elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka mitano na ilikuwa kazi ngumu kwake katika mwanzo wa masomo yake shuleni kutokana na kutoelewa lugha ya kiswahili jambo lililowalazimu walimu kutafsiri masomo ya Kiswahili kwenda Kingereza ndani ya miezi miwili.

“Wazazi wangu wote wanazungumza lugha ya kingereza nami pia, shida nilianza kuiona nilipofika Tanzania na kuanza elimu ya msingi ilikuwa shida sana kwani masomo yote yanafundishwa kwa lugha ya taifa ya Kiswahili kasoro somo moja tu la kingereza lakini nilijifunza kiswahili na mitihani ya kuingia darasa la pili nilikuwa mwanafunzi wa kwanza.” Alisema Vaishnavi.

Mtihani wa darasa la pili kwenda darasa la tatu nilishika nafasi ya pili wakati darasa la pili kwenda la tatu nilishika nafasi ya kwanza huku darasa la tatu kwenda la nne pia kushika nafasi ya kwanza na mtihani wa taifa wa darasa la nne kwenda la tano pia kuongozwa kishule, kiwilaya Mvomero na mkoa kwa kushika nafasi ya kwanza.alisema Vaishnavi.

Matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la nne 2014  kwenda darasa la tano mwanafunzi huyo yameonyesha kupata alama 48 kati ya alama za juu 50 kwa somo la Kiswahili wakati English alipata alama 50-50 huku somo la histori, uraia na jiografia akipata alama 50-50.

Masomo mengine ni hisabati ambayo alipata alama 50-50, sayansi alama 42-50 huku somo la haina na michezo akipata alama 46-50 na kukusanya alama 282 kati ya alama za juu 300.

Akielezea mikakati yaliyomfanya awe mwanafunzi bora kishule, wilaya na mkoa kwa mwaka 2014, Vaishnavi alisema kuwa darasa la kwanza na pili alikuwa akitoka shule saa 6 mchana na baada ya kufika nyumbani alienda kuoga na kula kisha kulala kwa dakika 30 ama saa 1:00.

Baada ya kuamka Vaishnavi huchukua daftari na kujikumbusha alichofundishwa shule kwa muda wa dakika 30 au 45 na kuendeleaa na michezo.

Kuingia kwa darasa la tatu, ratiba ya kwenda shule na kurudi nyumbani ilibadilika, ambapo baada ya  kutoka shuleni saa 10 jioni saa 11 jioni aliendeleza tabia ya kusoma vitabu vya Kiswahili hasa vya darasa husika na saa 12 jioni hiyo hiyo kucheza na rafiki zake.alisemaVaishnavi.

Vaishnavi alisema kuwa baada ya michezo yake Saa 1:30 usiku huanza tena kusoma hadi saa 2:00 usiku huo kula chakula cha usiku na kwenda kulala.

Hali hiyo ilimsaidia Vaishnavi kuifahamu lugha ya Kiswahili kwa haraka zaidi kupitia michezo shuleni na wanafunzi wenzeke hata rafiki zake waliokuwa wanamteembelea nyumbani kwao walimsaaidia kumfundisha kiswahili.alisema Vaishnavi.

Wakati mungine alikuwa analazimika kulala saa 3:45 usiku baada ya kuangalia kipindi cha tamthilia cha Everest Plus kilichokuwa kinarushwa na luninga ya Azam TV ambapo shangazi yake, Shamata Anchan ambaye ni miss south India.


Meneja wa fedha kiwanda cha sukari cha Mtibwa, Vivek Sanil (45) ni baba wa mtoto huyo na mama yake ni meneja wa mali ghafi na vipuri katika kiwanda hicho, Amita Sanil (32) kwa pamoja walieleza namna walivyomsaidia katika malezi.

Sanil anasema kuwa katika malezi ya mtoto huyo wamekuwa na tabia ya kuwekeana zamu ya kumfundisha masomo yake kuanzia yeye, mama yake na msichana wa kazi.

“Huyu Vaishnavi kimsingi amepata malezi mazuri hasa kwa jamii iliyomzunguka, kuanzia sisi wazazi wake, msichana wetu wa kazi, hata meneja wetu wa kiwanda mr Yahaya kwa pamoja tumemsaidia kujua Kiswahili kwa nyumbani na kazi hiyo iliendelea shuleni pia.”alisema Sanil.

Mke wake alikuwa na kazi ya kumfundisha somo la kingereza, baba akiwajibika kumfundisha hisabati, msichana wao wa kazi alikuwa na kazi ya kumfundisha Kiswahili na baadhi ya masomo ya Kiswahili.

Meneja wa kiwanda cha Mtibwa sugar Hamad Yahaya aliwajibika kumfundisha masomo ya Kiswahili pindi alipokuwa akitembelea katika makazi ya familia hiyo.

MWALIMU MKUU:
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiwandani kata ya Mtibwa iliyopo tarafa ya Turiani wilayani Mvomero, Damian Joseph Kahimba anamwelezea mwanafunzi huo kuwa ni azina kubwa kwa dunia katika siku za usoni.

Vaishnavi amekuwa na misingi mizuri ya kielimu kutoka kwa wazazi wake na kazi kubwa kwa walimu ni kumjengea mifumo ya elimu iliyogota katika lugha ya taifa la Tanzania ambayo ni Kiswahili na tumefanikiwa”. Anasema Damian Kahimba.

Mwalimu Kahimba anasema kuwa, Vaishnavi ni mtoto mwenye kipaji, alianza kuonyesha maajabu kwa kushika nafasi za tangu akiwa darasa la kwanza hadi darasa la nne.

Alama za mtihani wa shule ya Kiwandani kwa mwaka 2014, Vaishnavi alipata alama 800 ambapo katika mtihani wa taifa wa darasa la nne kwa mwaka huo 2014 alishika nafasi ya kwanza, kiwilaya ya Mvomero nafasi ya kwanza ikiwa kuwapiku wanafunzi 7222 wa wilaya hiyo.

Mwalimu Kahimba anasema kuwa shule ya msingi Kiwandani-Mtibwa ina walimu wanaojituma na kutokana na hilo wamekuwa wakifanya vizuri wanafunzi katika mitihani ya taifa ya darasa la saba ambapo kwa mwaka 2006 walishika nafasi ya nne kiwilaya.

Mwaka 2007 nafasi ya tatu, mwaka 2008 nafasi ya pili, mwaka 2009 nafasi ya kwanza, 2010 nafasi ya tano, 2011 nafasi ya nne, mwaka 2012 nafasi ya tano, mwaka 2013 nafasi ya sita na mwaka 2014 wakashika nafasi ya pili kwa kufaulisha kwenda kidato cha kwanza kiwilaya.

“Kama shule itakuwa na madarasa ya kutosha, walimu wa kutosha, madawati, vitabu vya kutosha na wastani wa wanafunzi, kazi ya ualimu kumfundisha mtoto inakuwa rahisi kufundisha wanafunzi.”alisema Kahimba.

“Mwanafunzi wa darasa la kwanza asipopata misingi bora na imara, mwanafunzi huyo atapata shida katika madarasa mengine.”alisema Kahimba.

Kahimba alisema kuwa utaratibu wa shule yao mwanafunzi hawezi kwenda darasa nyingine bila kuwa na kiwango kizuri cha ufaulu wa darasa husika vinginevyo atarudia darasa.

“Darasa la kwanza hawezi kwenda darasa la pili bila kujua kusoma na kuandika hivyo hivyo darasa la pili pia hawezi kwenda darasa la tatu na madarasa mengine na alama zetu ni 350 afikie alama hizo ili avuke darasa na kwenda lingine.”alisema Kahimba.

MENEJA WA MTIBWA SUGAR.
Meneja mkuu wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa Sugar, Hamad Yahaya anasema kuwa kipaji alichonacho mtoto, Vaishnavi Vivek Sanil ni hazina inapaswa kuendeleza ili umma wa watanzania na dunia kiujumla ifaidike nayo.

“Nilipatwa na mshangao kwa namna mwanafunzi Vaishnavi katika matokea yake ya mwaka hasa mwaka wa kwanza ambayo Kiswahili kilikuwa tabu kwake lakini akashika nafasi ya kwanza lakini hii shule inamilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mtibwa na ameweka historia kwake na kiwanda pia.”alisema Yahaya.

Jina la Mtibwa limenyanyuliwa na mtoto huyo kutokana na ufaulu wake kwa kushika nafasi ya kwanza kishule, wilaya na mkoa wa Morogoro katika mtihani wa taifa wa darasa la nne ndani ya Tanzania na nje kwa kulitangaza vyema jina la kiwanda.”aliongeza Yahaya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: