BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TIMUATIMUA YA MAKOCHA MECHI YA SIMBA NA YANGA, YAMTIA KIWEWE NA HOMA KOCHA MKUU WA SIMBA SC.


Kocha wa Simba Goran Kopunovic akisimamia zoezi la Simba Zanzibar


Zanzibar.
Kocha wa Simba Goran Kopunovic ni kama ana wasiwasi mkubwa na mechi hiyo ambayo yeye ni mara yake ya kwanza kukutana na Yanga tangu achukue mikoba ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa Patrick Phiri aliyesitishiwa ajira yake kutokana na mwenendo mbovu.


Hali hiyo ilitokea visiwani hapa, Jumanne usiku wakati kocha huyo alipozungumza na wachezaji wake na moja ya mambo aliyoyasisitiza ni kuhakikisha wanaifunga Yanga ili naye alinde kibarua chake kisiote nyasi.


Goran anahofia yaliyomtokea kocha wa Yanga, Marcio Maximo aliyetimuliwa baada ya kufungwa na Simba mabao 2-0 kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 13 mwaka jana.


Habari kutoka ndani ya kambi hiyo, zinasema Goran amekuwa na wasiwasi na matokeo ya mechi hiyo na kulazimika kuwasisitiza wachezaji wake wacheze kwa kujituma ili kumlinda asipatwe na kadhia hiyo.


Kocha huyo amekuwa mgumu kuzungumzia mechi hiyo ambayo inaonekana kuwa na presha kubwa.


Hata hivyo, gazeti hili limebaini kwamba wachezaji wametokea kumkubali kocha huyo, hivyo njia anayotumia kwa sasa ni kuwahamasisha wajitume na kuifunga Yanga.


Hilo lilijionyesha kwenye mazoezi yaliyofanyika juzi, Jumatano jioni ambako wachezaji walionekana kuwa na morali ya hali ya juu.


“Kocha amezungumza nasi, unajua amepata historia ya kufukuzwa kwa Maximo, hivyo anaona kama mwenzake alifukuzwa kwa kufungwa nasi, je, ikitokea sisi kupoteza mechi hiyo itakuwaje kwake, hivyo anaamini pengine na yeye atafukuzwa kazi, tunapambana ili kuhakikisha Yanga hawatoki, tutamlinda kocha wetu kwani ana wasiwasi,” alisema mchezaji mmoja mwandamizi wa Yanga.


Jana asubuhi, Goran aliwapa mapumziko wachezaji wake baada ya juzi kufanya mazoezi mazito na hivyo jioni waliendelea na mazoezi yao kwenye Uwanja wa Amaan.


Goran alitua Simba baada ya uongozi wa klabu hiyo kusitisha mkataba na Phiri aliyeshindwa kutimiza malengo yake kutokana na timu yao kusuasua kwenye ligi.


Phiri aliiongoza Simba kuheza mecni nane na kati ya hizo alishinda mechi moja na nyingine kutoka sare.


Hata hivyo, Phiri alikutana na Yanga mara mbili kwenye Ligi Kuu, timu hizo zilitoka sare ya 0-0, huku akishinda mechi ya Mtani Jembe na kufukuzwa baada ya kufungwa na Kagera Sugar kwa bao 1-0.


Wakati kocha huyo akirudi kwao Zambia alitoa neno kwa Goran kuwa ili ajiwekee imani kwa wanachama, viongozi wa Simba ni lazima ashinde mechi yao na Yanga, itakayochezwa Jumapili.


Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 23 dhidi ya Yanga inayoongoza ikiwa na pointi 31.


Tayari, Simba wametamba kuwa watashinda mechi zao zijazo na kuwasimamisha Yanga.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: