BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOCHA MKUU WA YANGA SC AJIVUNIA KUWEKA REKODI YA TIMU YAKE KUFUNGA BAO 8-0 KATIKA MCHEZO MMOJA TANGU AANZE KUFUNDISHA SOKA.

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/Pluijm.jpg
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, ameeleza kuwa ameandika historia ya kwanza tangu aanze kufundisha soka, kwa timu yake kufunga mabao nane katika mchezo mmoja.



Yanga juzi iliitungua Coastal Union mabao 8-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuzidi kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuchukua ubingwa wa ligi, ikiwa na jumla ya pointi 43.


Wanajangwani hao wameandika historia ya pekee kwenye msimu huu wa ligi kwa kufunga idadi kubwa ya mabao, ambapo hakuna timu yoyote iliyoweza kufunga idadi hiyo na kuvunja rekodi yao wenyewe waliyoiweka msimu uliopita kwa kuifunga Ruvu Shooting mabao 7-0.


Akizungumza Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Pluijm alisema ni ushindi mkubwa sana kuupata, alikuwa na mategemeo ya kushinda, lakini ushindi huo umekuwa zaidi, si kitu kidogo walichokifanya wachezaji wake.


“Mabao yote yamefungwa vizuri, wachezaji walionyesha kiwango kizuri na niliona mabao mengi zaidi ya hayo, lakini walikuwa wanakosakosa, nimefurahi sana na siwezi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja, lakini wote wamenifurahisha,” alisema.


Alisema, amefurahishwa pia na Kpah Sherman kwa kufunga bao la kwanza akiwa ametokea kwenye majeraha, amejaribu na amefanikiwa.


Alisema, Coastal Union ni timu nzuri na ngumu, lakini bahati haikuwa yao, anasikitika kuwakosa wachezaji wake, Andrey Coutinho, Mrisho Ngassa na Hussein Javu, ambao ni majeruhi, kwani nao wangekuwa uwanjani huenda wangepata mabao zaidi.


Pluijm alisema, kazi iliyokuwepo sasa ni jinsi ya kupata ushindi mbele ya Mbeya City, ukiwa ndio mchezo wao unaofuata Jumapili hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


“Utakuwa ni mchezo mgumu, kwani timu tunayokutana nayo ni timu nzuri na ngumu, lakini tutahakikisha tunachukua ushindi mbele yao,” alisema.


Alieleza kwa sasa mpango wao ni kuchukua pointi kwa kila mchezo, hatimaye kuchukua ubingwa wa ligi, huku wakiwa na ndoto za kuchukua ubingwa pia wa Kombe la Shirikisho Afrika.


Wakati huo huo, timu ya Platnum ya Zimbabwe kupitia akaunti yao ya Twitter, imewapa hongera Yanga kwa ushindi huo mnono wa 8-0, wakiandika ‘Hongereni marafiki wetu wapya’.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: