BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TANZANIA YAHAHA KUSAKA WATU WAKE TUKIO LA UGAIDI CHUO KIKUU LILILOUA WATU 147 KENYA.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa tatu kushoto) akiwa kwenye misa ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana.(Picha na Fadhili Akida).

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, unafuatilia kama kuna wanafunzi wa Tanzania waliojeruhiwa au kuuawa katika shambulio la kigaidi, lililoua wanafunzi 147 wa Chuo Kikuu nchini humo.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Membe alisema ubalozi huo unatarajiwa kumpa taarifa mapema iwezekanavyo na leo atatoa taarifa kuhusu mauaji hayo, yaliyofanywa na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.

“Kuhusu suala hilo nitatoa taarifa kesho (leo) baada ya kupata taarifa rasmi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini humo….na nitajua nitatoa kwa kuita waandishi au kutuma taarifa tu,” alisema Membe aliyekuwa akitoka katika Misa ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph.

Alisema hajapata taarifa zozote, lakini ubalozi wa Tanzania nchini humo unaendelea kufuatilia kama kuna wanafunzi wa Kitanzania waliokuwa wakisoma chuoni hapo na kufa au kujeruhiwa.

Chuo kikuu hicho nchini Kenya kililipuliwa na magaidi wa kundi la Al-Shabaab na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa huku baadhi ya wanafunzi hawajulikani walipo.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: