YANGA SC YATOA KIPIGO CHA PAKA MWIZI KWA KUICHAKAZA COASTAL UNION BAO 8-0, AMIS TAMBWE AFUNGA BAO NNE UWANJA WA TAIFA.
Washambuliaji wa Yanga SC, Amis Tambwe na Simon Msuva kushoto wakishangilia baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 8-0 dhidi ya Coastal Union uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga walianza kupata mabao kupitia kwa mshambuliaji wao Amis Tambwe aliyefunga mabao manne katika dakika za 10, 33, 48, 90 + 1 huku Simon Msuva akifunga bao mbili dakika ya 24, 87.
Kpar Sherman akifunga bao moja dakika ya 49 wakati mchezo mungine wa ligi hiyo ya tanzania bara Azam FC ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika uwanja wake wa Chamanzi
Kwa matokeo hayo Yanga SC wameendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kukusanya pointi 43 huku Simon Msuva akiongoza kwa kufumania nyavu kwa kupachika bao 13.
0 comments:
Post a Comment