Kiungo wa Yanga SC Mbrazil, Andrey Coutinho ameifungia timu yake bao dakika ya 12 dhidi ya Azam FC kabla ya Azam FC kusawazisha.
Mchezaji wa Azan FC, Bryson Rafael aliisawazishia timu yake dakika moja tu baada ya Yanga SC kupata bao la kuongoza na kufanya mchezo huo umalizike katika ngwe ya kwanza kwa kutoshana nguvu kwa bao 1-1.
Mchezaji wa Azam FC Aggrey Morris amepachika bao la pili na kuifanya Azam FC iongoze dhidi ya Yanga SC bao lililopatikana katika dakika ya 76 na kuifanya Yanga SC ikubali kipigo cha bao 2-1 mbele ya Azam FC baada ya kumalizika kwa dakika 90.

0 comments:
Post a Comment