Juma Mtanda, Morogoro.
Mgomo ulioitishwa na madereva wa mabasi nchini uliendelea kuleta athiri kwa wananchi wenye kipato duni wakiwemo wanafunzi kushindwa kwenda shule kutokana na kushindwa kumudu ghalama za nauli kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Nauli hizo zilikuwa zikitozwa kiasi cha sh1,000 badala ya nauli ya awali ya sh200 kwa wanafunzi na watu wazima sh400 ambazo madereva wa gari ya kubeba mizigo na bajaji kusafirisha wananchi huku wengine kulazimika kutembea umbali mrefu mkoani Morogoro.
Mgomo huo umewalazimisha wakazi wa Manispaa ya Morogoro baadhi yao kutembea umbali mrefu na wengine kutumia kiasi kikubwa cha fedha kutoka sh8,00 hadi sh2,000 na kuendelea huku sehemu ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaosoma shule zenye umbali kuanzia kilometa tano had nane kurudi majumbani kwa kushindwa kumudu ghalama za nauli.
Wakizungumza na MTANDA BLOG kwa nyakati tofauti mjini hapa wakazi hao walieleza kuwa mgomo huo umeathiri kwa kiasi kikubwa na kueleza sio usafiri tu bali wanafunzi, waendesha pikipiki maarufu (Bodaboda) na wafanyabiashara wa bidhaa ndogondogo ikiwemo na wananchi wanaoishi pembezoni wa Manispaa ya Morogoro.
Mkazi wa Nyandila kata ya Mgeta wilaya ya Mvomero, John Manywele (46) alieleza kuwa alilazimika kutumia kiasi cha sh15,000 kama nauli kutoka Dar es Salaam kurudi Morogoro katika usafiri wa gari aina ya fuso kutokana na mgomo huo.
“Juzi nilikuwa Dar es Salaam lakini kutokana na mgomo huu nimelazimika kulipa nauli kiasi cha sh15,000 kwa kupanda katika fuso na leo hii napanda hii pikipiki kwa kulipia kiasi cha sh15,000 kutoka Morogoro mjini kurudi kwetu Nyandila Mgeta ambapo nauli ya basi ni sh4000 tu.”alisema Manyweli.
Mwendesha pikipiki stendi kuu ya daladala ziendazo nje ya Manispaa ya Morogoro, Stanley Ndunguru alieleza kuwa biashara za kupakia abiria katika stendi hiyo imekuwa mgumu kutokana na uhaba wa wateja wao.
Nduguru aliongeza kwa kusema kuwa wateja wao hata hao wachache wanaohitaji huduma ya usafiri wao wamekuwa wameporwa na gari ndogo, bajaj zilizosajiliwa kwa kubeba mizigo na gari binafsi kusafirisha abiria hao katika kipindi cha mgomo.
Naye Veronica Kagoma mfanyabiashara wa bidhaa ndogo ndogo alieleza kuwa amelazimika kufunga biashara yake kutokana na stendi kuu ya daladala kukosekana kwa abiria ambao ni wateja wao wakuu.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment