Watu sita wajeruhiwa baada ya bomu kurushwa kwa mkono wakati wakitoka katika maadhimisho ya Mei Mosi.
Hofu ya ugaidi imezidi kutanda katika wilaya ya kilombero baada ya watu sita kujeruhiwa vibaya na bomu lililorushwa kwa mkono wakati wakitoka katika maadhimisho ya Mei Mosi katika kijiji cha Msolwa ujamaa kata ya sanje wilayani kilombero mkoani Morogoro
.
Katika hospitali ya ST KIZITO MIKUMI walikolazwa majeruhi wa tukio hilo wamesema bomu hilo lilirushwa na vijana wawili baada ya kutiliwa shaka na wananchi wa kijiji cha Msolwa ujamaa kata ya sanje tarafa ya Mangula kuwaweka chini ya ulinzi kwa ajili ya kuwapekua.
Vijana hao walirusha bomu na kujeruhi wananchi pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa kwenye gari ya mweneyekiti wa halmashauri wakitokea katika maadhimisho ya Mei Mosi ambapo wameomba jeshi la polsi kufanya uchunguz kufuatia matukio yanayoashiria ugaidi kuendelea kuandama wakazi wa kilombero.
Nao viongozi wa kata akiwemo diwani wa kata ya sanje David Ligazio wamesema ipo haja ya serikali kuongeza nguvu ya jeshi la polisi ikiwa ni pamoja na magari ya usafiri na kutafuta vifaa vinavyo weza kuchunguza maeneo ya milima ya udizungwa na Ruaha ambapo wamebaini wahalifu wengi wamewaona wakitokea katika misitu hiyo mara kw amara.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Pual amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hadi sasa jeshi la polisi linawatafuta watuhumiwa hao ambao baada ya kurusha bomu hilo limejeruhi dereva wa mweneyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilombero na kuharibu gari ya halmshauri pamoja na wananchi wa kijiji cha msolwa ujamaa.
Tukio hilo limetokea ndani ya siku 14 baada ya watuhumiwa 9 kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi, bendera nyeusi pamoja na vitu mbalimbali vya kufanyia uhalifu huku mmoja akichomwa moto na wananchi wenye hasira akiwa katika harakati za kutoroka baada ya kumchoma askari kwa jambia shingoni katika tarafa ya kidadu wilayani kilombero.ITV
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / BOMU LAWALIPUKIA WATU SITA NA KUWAJERUHI VIBAYA BAADA YA KURUSHWA KWA MKONO WAKATI WAKITOKA KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI MORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment