HII SILAHA INAYOTUMIWA NA NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALLA JIMBO LA MVOMERO SIYO MCHEZO.
Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos makalla.
Mbunge wa jimbo la Mvomero wilaya ya Mvomero, Amos Makalla leo Mei 30 yupo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika tawi la Kidudwe tarafa ya Turiani mkoani Morogoro.
Silaha inayotumiwa na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makkala ya Utumishi bora, Uwajibikaji, Umoja na Uzalendo yenye lengo la kuwahamasisha wananchi kupenda kujenga umoja na uzalendo sanjari na uwajibikaji ni silaha inayopaswa kuunga mkono katika ngazi ya na wananchi wa Tanzania.
Utumishi bora, Uwajibikaji, Umoja na Uzalendo ikitumika vizuri hasa kwa wananchi wa wilaya ya Mvomero madhalani kufanyia kazi suala la kuibua miradi ya maendeleo ndani ya vijiji vyao itasaidia kupunguza baadhi ya changamoto ambazo wananchi wanakabiliana nazo na kuipunguzia serikali mzigo mzito wa kuwahudumia wananchi.
Dhamira kuu ya ziara hiyo ni kukagua miradi iliyopelekwa katika vijiji vya jimbo hilo na mbunge huyo sambamba na kuchochea juhudi za kuikamilisha kwa wakati chini ya kauri mbiu Utumishi bora, Uwajibikaji, Umoja na Uzalendo.
Makalla ni miongoni mwa wabunge walioonyesha nia kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kupitia chama chake cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu wa kuchagua madiwani, wabunge na nafasi ya urais.
Baadhi ya kazi za mbunge ni kukusanya kero na kuwasilisha katika vikao vya halsmashauri na bungeni ili serikali kuweza kutatua.
MTANDA BLOG inakaribisha matukio mbalimbali yaliyofanywa na viongozi wa umma, taasisi za serikali na binafsi wakiwemo madiwani, wabunge kuelezea ni namna gani wamefanikiwa katika kuwahudumia wananchi katika ngazi mbalimbali sambamba na changamoto wanazokumbana nazo.
0 comments:
Post a Comment