Wageni waalikwa kutoka nchi mbalimbali wakijadiliana jambo wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani katika kongamano lililofanyika mkoani Morogoro, Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika ardhi ya Morogoro chini ya kauli mbiu ya mwaka huu 2015 “Usalama
wa vyombo vya habari kwenye dhama za Digitali, Uandishi makini usawa wa
Jinsia na Faragha. PICHA/MTANDA BLOG.
Waandishi wakongwe wakiongozwa na Ndimala Tegambwake kulia wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Hawa ni wakongwe wengine Pili Mtambalike wa kwanza kushoto na wenzake nao wakifuatilia kongamano hilo.
Mwandishi mkongwe Eda Sanga akizungumza jambo wakati wa kongamano hilo.
Mratibu wa miradi chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MoroPc) Thadei Hafigwa naye akizungumza jambo
Mkurugenzi wa New Media and Digital Security Consultant, Maxence Melo kushoto akieleza jambo kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mjengwa Blog, Majid Mjengwa akieleza moja ya changamoto aliwahi kukumbana nazo wakati wa utekelezaji wa majuku yake ya kazi ikiwemo na makala mbalimbali alizowahi kuandikia katika magazeti mbalimbali ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Simon Berege akiendesha kongamano hilo akisaidiwa na mwandishi mkongwe Eda Sanga kushoto na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka
mwandishi mkongwe Eda Sanga na kulia ni Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Simon Berege.
Mwandishi mkongwe Ahmes Salimu akichangia moja ya mada iliyokuwa ikijadiliwa
Huyu ni Bujaga Kadago Lyango a.k.a Baba Askofu ambaye ni mtangazaji mkongwe naye akitoa uzoezfu wa kazi yake.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Ernest Sungura akieleza jambo kwenye kongamano hilo kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy akieleza jambo juu ya mitandao ya kijamii namna watumiaji wanavyoshindwa kuzingatia maadili hasa Tanzania.
Mlezi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (Moropc) na mwandishi mkongwe Steven
Mashishanga ambaye pia aliwahi kushika nyasfa mbalimbali serikali ikiwemo cheo cha ukuu wa Mkoa akipitia ndoo wakati wa kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa New Media and Digital Security Consultant, Maxence Melo akitoa ushuhuda juu ya matukio mbalimbali yaliyomkumba kutokana na mijada iliyowahi na inayoendelea kujadiliwa katika jamii forums wakati wa kongamano hilo, Chini ni bango ambalo lina ujumbe likionekana moja ya mitaa ya Marekani.
Mwenyekiti wa Morogoro Press Club kushoto Idda Mushi na Mweka Hazina wake Lilian Lucas ambao ni wenyeji wa kongamano hilo la siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari dunia nao wakifuatilia matukio yalikuwa yakiendelea.
Mtangazaji mkongwe Masoud Masoud akieleza jambo katika kongamano hilo.PICHA/Mtanda Blog.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment