POINTI SITA ZAMALIZA UBISHI KATI YA FLOYD MAYWEATHE NA MANNY PACQUIAO
Pambano la ngumi za kulipwa kati ya Floyd Mayweathe na Manny Pacquia limemalizika kwa Mmarekani Mayweather kushinda kwa pointi sita dhidi ya mpinzani wake Mphilipino Pacquiao baada ya pambano hilo kumalizika kama chati inavyoonyesha hapa chini.
Floyd ameibuka na pointi 117 alizopewa na majaji kutokana na kurusha vyema makonde yake dhidi ya mpinzani wake wakati Pacquiao yeye ameambulia pointi 111 zilizomfanya ashindwe kuibuka mbabe dhidi ya Floyd.
Pambano hili limekuwa la kihistoriakwa dunia nzima ililazimika kusubri kuona nani kati ya bondia Floyd ‘Money’ Mayweather na Manny Pacquiao ataibuka mshindi lakini kitandawili hicho kimetenguliwa.
Pambano lilikuwa raundi 12, ambapo Floyd Mayweather amefanikiwa kumshinda Pacquiao kwa pointi hizo sita tu na kuamua mbabe kati yao ni nani.
0 comments:
Post a Comment