BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAKATA LA WANAWAKE WA ROMBO KUKODI WANAUME KUTOKA NCHINI KENYA KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA YA UNYUMBA SASA IMEFIKIA HAPA.

  
MADAI ya wanawake wa wilaya ya Rombo, Kilimanjaro, kukodi wanaume kutoka nchini Kenya, baada ya kukosa huduma za ndoa kutoka kwa waume zao kwa muda mrefu, kutokana na ulevi wa gongo uliopindukia, zimemfadhaisha Mbunge wao, Joseph Selasini (Chadema).

Mbunge huyo amefikia hatua ya kusema kuwa familia yake na wananchi wa huko, wamefadhaika na kuingiwa na wasiwasi kuwa huenda wenzi wao katika ndoa zao ikiwemo ya mbunge, si waaminifu.

Selasini alisema hayo Bungeni, alipokuwa akiuliza swali kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambapo alisema ingawa hali hiyo imewafadhaisha, lakini alitetea utengenezaji wa pombe za kienyeji, ikiwemo pombe haramu ya gongo.

Katika utetezi huo, Selasini alitaka Serikali iangalie namna ya kusaidia uboreshwaji wa pombe za kienyeji, kwa kuwa kipato chake kimekuwa kikisaidia ada za watoto, kujikimu na kuongeza kipato cha familia.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema kwa namna Selasini anavyozungumza, huenda anatetea suala la kuhalalisha pombe haramu aina ya gongo, na kama ndio hiyo Serikali itaendelea kupiga vita utengenezaji na matumizi ya pombe hiyo kwa sababu viwango vyake havipimiki.

“Mheshimiwa Selasini, kwa maelezo yako utakuwa unazungumzia gongo, sasa hii ni pombe haramu na Serikali inaendelea kuipiga vita kwa kuwa viwango vyake havipimiki.

“Lakini huenda kwa siku zijazo, jambo hili linaweza kuangaliwa na kiwanda cha Konyagi kuhusu namna ya kuiboresha kwa sababu hata Konyagi ni jamii ya gongo, lakini inapimika na haina madhara makubwa kwa watumiaji,” alisema Pinda.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwOYUvbsE09WOso1qO2ST1SW-CCwRvqMxgNfUR09vfZSeNeG-Rb5tO9lKkLrWB8PIhzH0lbCwRSFP1BQsSBHjCcQTy8MpCDsmX7CFbUDXMeEmnKVTnvgKTlJqMmnaggGQS7h6XPcy-Rnf-/s640/selasini+%25281%2529.jpg

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini.

Hata hivyo, katika swali la nyongeza la mbunge huyo, alimtaka Waziri Mkuu kukanusha tuhuma za Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Lembrice Kipuyo alizotoa wiki iliyopita akidai kuwa wanawake wa wilaya hiyo, wanakodisha wanaume kutoka nchi jirani ya Kenya kwa ajili ya kuwahudumia mahitaji ya kimwili, kwa kuwa waume zao wameshindwa kutokana na ulevi uliopindukia.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunaomba kauli ya serikali kuhusu jambo hili, na mkanushe taarifa hizo kwani zimeleta mfadhaiko kwenye familia na hata familia yangu, wanandoa wana wasiwasi kwamba wenza wao wanatoka nje ya ndoa, lakini pia kauli hiyo ni ya kudhalilisha wananchi wa Rombo”, alisema Selasini.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema hajasikia tuhuma hizo ;na kwamba kama zimetolewa na Mkuu huyo wa Wilaya ni vyema aliyetoa, azikanushe mwenyewe kwa kuwa ndiye anayejua alizitoa katika mazingira gani na wapi.

Aidha, alisema ni vyema apewe muda wa kulifahamu jambo hilo ;na kusema ataiagiza Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuangalia jambo hilo kama Mkuu huyo wa Wilaya alichokisema, sio sahihi ili hatua nyingine zifuate.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila alimuuliza Waziri Mkuu atoe kauli ya serikali kuhusu kukwama kutolewa kwa fedha za wahisani kwenye bajeti ya serikali, kutokana na wahisani hao kugoma kwa madai ya sakata ya akaunti ya Escrow.

Hatua hiyo imesababisha fedha za Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) awamu ya pili, hazijasainiwa na kusema Waziri wa Fedha awali alilidanganya Bunge kuwa fedha hizo zimeshasainiwa na kutaka serikali kutoa kauli juu ya kauli ya uongo ya waziri huyo.

Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema suala la Waziri wa Fedha kusema uongo sio lake, bali la Bunge na hivyo Bunge ndilo lenye jukumu ya kuchukua hatua, ikiwa waziri huyo alilidanganya Bunge na kwamba tatizo la ufinyu wa bajeti ya nchi, halitokani tu na wahisani kusitisha fedha zao kwa sababu ya sakata la Escrow, bali ni la muda mrefu.

“Nijibu hili la ufinyu wa bajeti, sio kweli kwamba sakata la Escrow ndio chanzo kikuu, miaka mitatu sasa na zaidi wahisani wameendelea kusuasua kutoa fedha zao, ndio maana serikali imeamua sasa kujikita zaidi kuangalia vyanzo vya ndani vya mapato zaidi kuliko kuwategemea hao”, alisema Pinda.

Kuhusu kauli ya Waziri wa Fedha kulidanganya Bunge juu ya kusainiwa kwa awamu ya pili ya fedha za MCC, kutokana na sakata la Escrow, Pinda alisema waziri husika atalitolea ufafanuzi bungeni.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: