BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MATUKIO NDANI YA MANISPAA YA MOROGORO MEI 12/ 2015

 
Basi ndogo aina ya coasta likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali eneo la Mkundi barabara kuu ya Dodoma-Morogoro likiwa kituo kikuu cha polisi mkoani Morogoro, basi hilo lilibeba maiti waliotokana naye Dar es Salaam wakielekea mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi, ambapo katika ajali hiyo watu wawili warifaki dunia hapo hapo katika tukio lililotokea mwisho mwa juma.PICHA/MTANDA BLOG.




Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd mkoa wa Morogoro, Hamida Shariff akiwa amempakata mtoto wake mchanga baada ya kujifungua katika hospitali ya rifaa mkoa huo kwa njia ya operesheni baada ya kushindikana kujifungua kwa njia ya kawaida mkoani hapa.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiangalia ajali iliyohusisha daladala na mkokoteni katika barabara ya Korogwe, hata hivyo mwendesha mkokoteni alinusurika kuumia Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro Juma Bilal maarufu kwa jina la Kamuzu akiwa chini ya ulinzi wa wananchi baada ya kumtuhumu kuiba gurudumu na vifaa vingine vya gari vinavyodaiwa kufikia thamani ya zaidi ya sh2 milioni baada ya kumkamata mtaa wa Mtawala mkabala na gereji ya Hoood mkoani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: