TETEMEKO LAIKUMBA TENA NCHI YA NEPAL, LASABABISHA VIFO ZAIDI YA WATU 8,000.
Tetemeko kubwa la Ardhi limetikisa tena Nepal ,takriban majuma mawili tu tangu tetemeko lingine kubwa zaidi kusababisa vifo vya zaidi ya watu 8000.
Watafiti wanasema kuwa kitovu cha tetemeko hilo lililikuwa katika mji wa Namche Bazar, karibu zaidi na mlima mrefu zaidi duniani Mlima Everest.
Kulingana na idara ya maswala ya ardhi na mazingira ya Marekani tetemeko hili lipya limefikisha kipimo cha 7.4.
Tetemeko la awali lililotokea tarehe 25 Aprili , lilisajili vipimo vya 7.8.
Madhara ya tetemeko hili hayajabainika ila inasemekana kuwa lilitikisa mji mkuu wa India New Delhi, vilevile mji mkuu wa Bangladesh Dhaka.
Majumba yaliyosazwa na tetemeko la awali katika mji mkuu wa Nepala Kathmandu, yalitikiswa mno na tetemeko hili la hivi punde.
Kulingana na walioshuhudia maelfu ya watu waliokuwa ndani ya majumba yao walitorokea sehemu za wazi hofu ikitanda kuwa madhara na vifo zaidi yatatokea.
''Jamani mungu atuokoe maanake tetemeko hili la hivi punde lilikuwa lakutisha zaidi.
lilikuwa kubwa mno ''anasema Prakash Shilpakar mkaazi wa Kathmandu.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa sita adhuhuri saa za Kathmandu.
Kitovu cha tetemeko hilo inadaiwa kuwa takriban kilomita 83km Mashariki mwa Kathmandu, eneo lililoko karibu na mpaka wa China.BBC
0 comments:
Post a Comment