BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YAWATAKA WAFUGAJI KUSAJILI MIFUGO.

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/11/NGOMBE.jpg 

Wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi imewahimiza wafugaji nchini kusajili mifugo yao ili iwe rahisi kwa serikali kujua idadi ya mifugo iliyopo na kufahamu mahitaji ikiwemo kumudu uagizaji wa madawa.


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo Na Uvuvi Dk Titus Kamani alisema hayo mjini morogoro wakati akizungumza na wadau wa sekta ya nyama waliokutana kuelimishana na kuhamasishana juu ya sheria mbalimbali ikiwemo ya nyama.

Dk Kamani alisema iwapo serikali itakuwa na takwimu sahihi na za kutosha watamudu upatikanaji wa madawa na masoko ya nje na ndani ya nchi.

Alisema katika masoko ya kisasa wanunuzi hutaka kujua nyama ilikotoka na kwa mfugaji wa aina ipi,na kusisitiza jamii kuachana na fikra potofu kuwa serikali inasajili mifugo ili kuichukua.

Kwa upande wake mwakilishi wa katibu mkuu kutoka wizara ya wizara Mifugo na Uvuvi,Tabu Chando alibainisha namna walivyo fanikiwa tangu kutungwa kwa sheria ya nyama ikiwemo kuandaa miongozo na kanuni bora za ufugaji pamoja na kuwepo ufugaji wa kibiashara.


Mkuu wa mkoa wa morogoro Dk Rajabu Rutengwe alisema bado nyama ya hapa nchini imeendelea kuuzwa ikiwa chini ya viwango na ile yenye viwango ikiuzwa kwa bei ya juu.

Dk Rutengwe alisema kwamba ipo haja ya kuboresha mfumo mzima wa ufugaji ili kuboresha uchumi wa wafugaji pamoja na taifa kwa ujumla.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: