MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA, VYAVITAKA VILABU VYA SOKA LIGI KUU KUWALIPIA KODI WACHEZAJI NA MAKOCHA.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeviagiza vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu ya nchini (mpira wa kulipwa) Tanzania, kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kutokana na kuajiri makocha na wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Kamshina wa TRA ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa katibu mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu nchini vinavyoajiri walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wahakikishe wanaweka kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia kuwaajiri.
Vilbu vya vinapaswa kuwasilisha mikataba yote ya ajira ya wachezaji na walimu wao ili kukokotoa kodi stahiki kwa kila mmoja wao na mikataba yao kugongwa muhuri na stempu.
Kwa mujibu wa sheria za Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kufungu namba 7, kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.
Aidha kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa stempu ya mwaka 1973, kifungu namba 5 kikisomwa pamoja na jedwali la sheria hii, kila mkataba unatakiwa kugongwa muhuri na stempu na ofisa wa stempu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Kwa kuwa TFF ndio mlezi na msimamizi mkuu wa vilabu vya Mpira wa Miguu hapana nchini na hasa Ligi Kuu, tunaviomba vilabu vyote kuhakikisha vinawasilisha mikataba ya walimu na wachezaji yao ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kugongwa mihuri na stempu.
U15 KWENDA MBEYA KESHO
Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kesho ijumaa kinatarajia kusafiri kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu kombani ya mbeya U15.
U15 ambayo inanolewa na kocha Bakari Shime, itaondoka na kikosi cha wachezaji wa thelathini (30) ambapo wanatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombani ya mkoa wa Mbeya ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.
Timu itacheza michezo ya kirafiki siku ya jumapili na jumatatu ambapo kocha Shime atatumia nafasi hiyo kutambua uwezo wa wachezaji wake na kuongeza wachezaji wengine watakaonekana kutoka katika kombani ya mkoa wa Mbeya.
Mwezi ujao kikosi cha U-15 kitaelekea kisiwani Zanzibar kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombaini ya Zanzibar kisha baadae kuendelea na ziara ya kucheza michezo ya kirafiki katika mikoa ya Iringa, Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza na Dodoma.
Lengo la TFF ni kuhakikisha Tanzania inakua na kikosi bora cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
TANZANITE YAINGIA KAMBINI
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite Stars, imeingia kambini jana jioni Mbande jijini Dar es salaam na itakua ikifanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.
Kikosi cha wacheaji 22 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage kinafanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwnaja wa Azam uliopo Chamazi kujiandaa na mchezo dhidi ya U-20 ya Zambia utakaofanyika kati ya tarehe 10, 11 na 12 July jijini Dar es salaam.
Mchezo huo dhidi ya Zambia ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Dunia wenye umri chini ya miaka ya 20, zitakazofanyika nchini Papua New Guinea mwaka 2016.
Wachezaji waliopo kambini ni, Najiati Abbasi, Zuwena Aziz, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Tatu Iddy (Evergreen Queens), Niwael Khalfani, Maimuna Hamis (Mburahati Queens), Anastazia Anthony, Amisa Athumani, Amina Ramadhani, Neem Paulo (JKT Queens).
Wengine ni Asha Shaban, Rebeka Daniel, Brandina Wincelaus (Tanga), Happines Hezroni, Jane Cloudy (JKT Queens), Wema Richard, Gerwa Lugomba, Sadda Ramadhani (Uzuri Queens), Anna Hebron (Evergreen Queens) na Shehati Mohamed (Mburahati Queens)
Aidha wachezaji Monica Henry, Tumaini Michael (Uzuri Queens), Diana Msewa (Mbeya), na Vailet Nicolaus (Evergreen) bado hawajaripoti kambini wanaombwa kuripoti na kuungana na wenzao katika maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zambia.
0 comments:
Post a Comment