TASWIRA YA ZITTO KABWE, KUUNGUA KWA SOKO KUU NA MKUTANO WA ACT MASASI MKOANI MTWARA.
ACT Wazalendo inaendelea na mikutano yake leo ambapo mchana huu mapori yanafyekwa Masasi, Mtwara.
Tunazidi kuwafikia watanzania wengi zaidi kwa shabaha kuu ya kuwafikishia Azimio la Tabora ambalo limehuisha misingi mizuri ya lililokuwa Azimio la Arusha.
Watanzania wanaendelea kupuuza propaganda na upotoshaji wanajitokeza kwa wingi wanasikiliza siasa za hoja na wanajiunga na timu ya wazalendo ili wawe sehemu ya historia ya mashujaa waliolirejesha taifa kwenye misingi ya kuasisiwa kwake.
Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Utu, Uadilifu, Hifadhi ya Jamii, Udugu, Umoja, Demokrasia, Kujitegemea, Juhudi na Bidii katika kazi ndio misingi tunayoihubiri.
0 comments:
Post a Comment