MBIO ZA KUSAKA WADHAMINI NAFASI YA URAIS KWA UPANDE WA EDWARD LOWASSA HII SASA NI KUFURU TUPU.
Mh. Lowassa akipokea fomu hizo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini Magdalena Daniel Ndwete.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akionyesha furaha, wakati katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini, Magdalena Daniel Ndwete, alipotangaza wana CCM 22, 758 kutoka mkoa wa Singida, wamemdhamini katika harakati zake za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia CCM, kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa alikuwa mkoani Singida, Jumanne Juni 16, 2015 kutafuta wadhamini kabla ya kuelekea Shinyanga ambako alishiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba.(Picha zote na K-VIS MEDIA)
Mh. Lowassa, akiangalia lundo la fomu za wana CCM mkoani Singida waliomdhamini
Mbunge wa viti maalum, kutoka mkoani Singida, Diana Chilolo, akipiga vigelegele wakati Mh. Lowassa, akitoa hotuba ya shukrani baada ya kupata idadi kubwa ya wadhamini
Wana CCM wa wilaya ya Singida mjini, wakijaza fomu hizo za udhamini Juni 16, 2015, kwenye ofisi za CCM mkoani humo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (NEC), Kampala Thomas Maganga, akizungumza wakati Mh. Lowassa alipofika mkoani Singida kutafuta wadhamini. Kulia ni Mjumbe wa NEC, kutoka mkoani Mwanza, Dkt. Raphael Chegeni
Mh. Lowassa, (mwenye nywele nyeupe), akiwasa,limia maefu ya wana CCM na wananchi wa Manispaa ya Singida, wakati akiwasili ofisi kuu za chama hicho kutafuta wadhamini
Mh. Lowassa akitoa hotuba ya shukrani.
0 comments:
Post a Comment