MWANDISHI APIGWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI.
Mwandishi wa Habari aliyefahamika kwa jina la, Omar Ali mkazi wa Mkoani Kangani kisiwani Pemba, jana majira ya asubuhi ameshambuliwa na kupigwa na askari wa jeshi la Polisi Zanzibar na kutupwa maeneo ya Maisara mjini humo.
Mwandishi huyu alikuwa anachukua habari katika kituo cha uandikishaji dafatari la kudumu maeneo ya Migombani Zanzibar na polisi hao inasadikiwa walimdhania kuwa ni mwandishi wa Chama cha Wananchi CUF.
Askari hao wanadaiwa walimshika na kuanza kumsulubu hali iliyopelekea kumjeruhi na kumvunja miguu.
Baada ya kipigo hicho mwandishi huyo alikimbizwa hospitalini na kugundulika miguu imevunjika huku akiwa hajitambui.
Ikumbukwe:
Matukio haya yanakuja baada ya wananchi wa Zanzibar kuhakikisha kila kituo hawezi kuandikishwa mtu ambaye hahusiki kama ambavyo tumeona na kuskia kupitia vyanzo mbali mbali.
Chanzo:http://www.jamiiforums.com
0 comments:
Post a Comment