RAIS WA SUDAN KUKAMATWA KAMA KUKU NCHINI AFRIKA YA KUSINI KWA AGIZO LA MAHAKAMA YA UHALIFU WA KIVITA YA ICC.
Mahakama moja nchini Afrika Kusini imeamuru rais wa Sudan Omar al Bashir asiondoke nchini humo.
Mahakama hiyo imemuagiza kusalia Afrika Kusini hadi itakaposikiza kesi iliyowasilishwa mbele yake ya kuitaka iamrishe serikali ya Afrika Kusini kumtia mbarani iliawasilishwe mbele ya mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya ICC iliyoko Hague Uholanzi.
Rais Al-Bashir yuko mjini Johannesburg, Afrika Kusini, kuhudhuria mkutano wa muungano wa nchi za Afrika ambao unaanza leo Jumapili anatafutwa na mahakama ya ICC kutokana na makosa ya kivita na mauaji ya halaiki.
Muungano wa Afrika umekiuka maombi kadha ya kuitaka imkamate al Bashir katika miaka ya awali.
Hata hivyo Afrika Kusini ambayo ni mwanachama wa ICC inawajibu wa kutekeleza amri za mahakama hiyo na hivyo inaweza kumtia mbaroni al Bashir.
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ilikuwa imeiagiza serikali ya Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan Omar Al-Bashir.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado zipo.
Rais al Bashir anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.BBC
0 comments:
Post a Comment