SERIKALI YAWAKUMBUKA WASTAAFU, SASA KUKENUA MENO KILA MWEZI.
Baadhi ya wazee wastaafu waliopigana vita ya mwaka 1978 kati ya Uganda na Tanzania.
Serikali kupitia Waziri wa Fedha leo Bungeni ametangaza kima cha chini kimeongezeka kwa wazee kwa asilimia 100.
Kuanzia Julai Mosi 2015 wazee wote wataanzwa kulipwa Shilingi laki moja.
Hatua hii imefikiwa kutokana na mapendekezo ya Wabunge wengi wakati wanachangia Bajeti kuu, kuiomba serikali iongeze Kima cha chini kifikie Shilingi za Tanzania laki moja, kutokana na ugumu wa maisha na mfumuko wa bei.
0 comments:
Post a Comment