Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.
“Tumekua na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.
Naye mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.
Washiriki wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu.
Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015.
STARS YAANZA MAZOEZI
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.
Stars inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded Morocco, itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.
Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na leo wamefanya mazoezi asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa na Mudathir Yahya (Azam FC).
TFF YAVIAGIZA VYAMA VYA MKOA KUWA NA VITUO VYA MPIRA WA MIGUU
Kufuatia pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na kukuza vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17.
Kwa mikoa ambayo tayari ina kituo ambacho inakiendesha yenyewe TFF inaonba ipatiwe taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kufahamishwa jina la kituo, jina la mwalimu na sifa zake na utaratibu wa mafunzo.
Kwa mikoa ambayo haina kituo TFF inagiza mikoa hiyo kuingia ubia na kituo kimoja ambacho tayari kina program ya kukuza na kuendeleza vipaji ili kijulikane kuwa ni kituo maalum cha mkoa husika.
Katika hilo TFF inaagiza kamati ya utendaji ya mkoa husika iandae muhtasari wa kikao cha utendaji cha chama cha mkoa wa kupitisha maamuzi hayo, MoU (makubaliano rasmi) yasainiwe kati ya chama cha mkoa na kituo husika na hati hiyo nakala yake iletwe TFF.
MoU hiyo ionyeshe majukumu ya chama cha mpira cha mkoa kama kutoa vifaa, kutoa mwalimu, usimamizi nk na pia kuonyesha majukumu ya mwenye kituo kama kutoa uwanja,ulinzi nk. MoU itaonyesha pia nani atafaidika na vipaji vitakavyoibuliwa kati ya mzazi,kituo na chama cha mkoa.
TFF itaandaa MoU ya mfano kwa ajili ya vyama vyote vya mikoa na ingependa kufikia tarehe 31/Desemba/2015 kila mkoa uwe umetekeleza jambo hilo.
SITA ZAPANDA DARAJA KUCHEZA SDL
Abajalo FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.
Timu hizo zimepanda daraja baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya Lindi, Manyara na Rukwa na kushirikisha jumla ya timu 27.
SDL inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.
Kundi A lina timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam), Milambo FC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Transit Camp (Dar es Salaam) wakati Kundi B ni AFC (Arusha), Alliance FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC (Arusha) na Pamba SC (Mwanza).
Timu za kundi C ni Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Kariakoo FC (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).
African Wanderers ya Iringa, Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Sabasaba United FC (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma) na Wenda FC ya Mbeya ndizo zinazounda kundi D.
Dirisha la usajili wa wachezaji limeshafunguliwa tangu Juni 15 mwaka huu, na litafungwa Agosti 6 mwaka huu.
VILBU VPL VYATAKIWA KUWASLISHA MAJINA YA MAKOCHA WA MAKIPA
Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu nchini (TFF) linaviomba vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuwasilisha jina la kocha wa magolikipa kufikia jumatatu ya tarehe 29 Juni, 2015 katika ofisi za TFF.
TFF imeandaa kozi ya magolikipa hivyo inahitaji kupata jina la kila kocha wa magolikipa ili kuweza kushiriki kwenye kozi hiyo itakayoanza tarehe 13 - 17 Julai, 2015 jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment