BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAFUNZI WAGUNDUA MIPIRA YA KIUME WENYE UWEZO WA KUTAMBUA MWANAMKE MWENYE MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA ZINAA KABLA YA KUJAMIANA NAYE.

 
Wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenyu

Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.


Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

nullKondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono. 

 Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.

Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

''tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.

Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .

Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''

''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''

Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.

Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa

"Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu''.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: