BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EDWARD LOWASSA AWAGOMBANISHA WANACCM ?. NAPE NNAUYE AMWELEZA KINGUNGE NGOMBALE-MWIRU AFANYE ANACHOTAKA KUFANYA

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1641452/highRes/436044/-/c46j67z/-/nape.jpg Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka mwanasiasa mkongwe, Kingunge-Ngombale Mwiru kufanya anachotaka kufanya.


Juzi Kingunge alijitokeza hadharani na kuzungumzia na waandishi wa habari huku akiwaambia kwamba kilichofanywa na CCM katika kumpata mgombea wa urais, Dk. John Magufuli ni haramu.

Dalili ya CCM kupasuka vipande zimeanza kuonekana dhahiri, baada ya Kingunge kujitokeza hadharani kupingana na maamuzi yote yaliyofanywa hususani kukata jina la Edward Lowassa katika hatua za mwanzo za kuteua mgombea urais.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0_w7lwiYpFOEqdUULfyqkeftD7DnIFr2aogqVNmYLMrdhoFNBrx5RWsSWOvNW2Cksmh351RaoFX6bqY6-_oOeo9OlM-LPG9Bx6_W6fo9y4MRpKRdrlXFr798FMghoLkHiyPiTKlnJgmE/s640/MMGL0629.jpg 
Edward Lowassa
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (pichani), akizungumza na NIPASHE jana kuhusu tuhuma zilitolewa na Kingunge ambaye kadi yake ya uanachama ni namba nane, alijibu kwa kifupi kwamba afanye anachotaka kufanya na kwamba hana maoni zaidi.

“Sina Comment (maoni) wewe unataka niseme nini? kaandike hivyo nilivyosema kwa sababu na mimi ni mwandishi na nilishawahi kuwa mhariri kwa hiyo najua,” alisema na kukata simu.

Chama hicho tawala kilimteua Dk. John Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wake mwenza kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwakani.
 
Kingunge Ngombale-Mwiru
 
Jumla ya watia nia 38 majina yao yaliingia katika vikao vya awali, lakini waliovuta kuingia tano bora ni Magufuli, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ali, Januari Makamba na Bernard Membe.

Hata hivyo, Halmashauri Kuu (NEC) iliwachuja Makamba na Membe na kuwabakiza Magufuli, Amina na Migiro kisha Magufuli kuibuka mshindi. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: