BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UNAPOKUWA CHINI YA ULINZI KWA KUTUHUMIWA JAMBO, HAYA NDIYO MAMBO YA MSINGI YA KUFANYA IKIWEMO KUMHOJI ASKARI ANAYEKUSHIKA KABLA YA KWENDA KITUONI.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVOLblYHaGBpa7un8LhAPF6Y8ncZxdB1wv1O1-GzpsgkC2YJ5-5s7pEsu0utzUNyUKrEfhCjqh6i-CTR9DUV6aJlo5lC0R9Aah0hqeZy4Pj-LT-st0o434b66to79JCjLvQIZH1q6AxumB/s1600/2.jpg 

Askari polisi akiwa amemshika mchezaji wa Yanga SC, Simon Msuva hivi karibuni katika picha ya maktaba.

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize
kitambulisho ni haki yako.


2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho
chenye muhuri wa mahakama kama anasema
ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini
anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki
yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata
kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya
kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji
anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga
naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo,
kukushika suruali kama hujakataa kukri amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine
baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila
kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na
ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo
kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au
uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1
jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla
hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa
mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima
kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki
salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke
na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo
taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka
unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki
yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho
hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika
mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu
uwapo chini ya ulinzi.


HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE
USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.
MIKONONI MWA POLISI, IMEANDALIWA NA MAWAKILI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: