BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MLINZI WA AZAM FC NA TAIFA STARS SHOMARI KAPOMBE AANZISHA LIGI YA VIJANA MORO.


Mwamuzi wa mchezo baina ya Masubo FC na Wakubeti FC, Shabaan Juma akitoa huduma ya kwanza kwa mchezaji Charles Sehoza baada ya kugongana na mwenzake Yahaya Machupa wa timu ya Wakubeti FC anayepatiwa huduma na Kalemuka Ahmed wakati wa ligi ya kugombea seti ya jezi mashindano ya Kapombe Cup 2015 hatua ya robo fainali iliyofanyika uwanja wa Sabasaba Morogoro, Masubo ilishindwa bao 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kutoa sare ya 0-0. PICHA/MTANDA BLOG.
Mshambuliaji wa timu ya Masubo FC, Awadhi Ahamadi kulia akiwania mpira na mlinzi wa timu ya Wakubeti FC, Paul Mgaya wakati wa ligi ya kugombea seti ya jezi mashindano ya Kapombe Cup 2015 hatua ya robo fainali iliyofanyika uwanja wa Sabasaba Morogoro, Masubo ilishindwa bao 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kutoa sare ya 0-0.PICHA/MTANDA BLOG.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mlinzi wa klabu ya Azam FC na Taifa Stars, Shomari Kapombe ameanzisha ligi ya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) yakiwa na lengo la kuvumbua vipaji vya wachezaji chipukizi mkoani Morogoro.

Wachezaji hao watapata fursa ya kucheza soka katika timu B za klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara mjini hapa.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, kaka wa Shomari Kapombe, Denis Kapombe alisema kuwa kwa sasa yeye amepewa jukumu la kusimamia michezo ya ligi ya Kapombe Cup 2015 ambayo imefikia hatua ya robo fainali katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya mkoani Morogoro.

Denis alisema kuwa ligi hiyo ilianza kutimua vumbi Juni mwaka huu katika uwanja wa shule ya msingi Mafiga kwa michezo ya hatua ya makundi na sasa hatua ya rono fainali, nusu fainali na fainali itafanyika kwenye uwanja huo wa Sabasaba.

“Mdogo wetu Shomari ameanzisha ligi yenye lengo la kupata vijana watano chini ya umri wa miaka 20 kila mwaka kuoitia mashindano haya wenye uwezo wa kucheza soka ili wapate nafasi za kucheza katika klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara ama ligi daraja la kwanza hii ikiwa sehemu ya kusaidia kuinua soka la tanzania sambamba na kuibua vipaji vilivyojificha”.alisema Denis.

Denis alisema kuwa Shomari alianzisha mpango huo wa ligi tangu mwaka 2014 na tayari vijana watatu wamefaidika nao kwa kujiunga na vikosi vya timu B vya klabu za Simba SC na Azam FC.

“Kuna mafanikio tayari Shomari ameanza kuyapata kwa kuwapeleka vijana watatu katika vikosi B, ambapo wachezaji wawili wamejiunga na klabu ya Simba SC huku Azam FC akipelekwa mmoja na katika ligi inayoendelea ambapo katika ligi inayoendelea wachezaji watano watachaguliwa na kupelekwa katika timu kubwa”.alisema Denis.

Katika ligi hiyo, timu ya Masubo FC ilifanikiwa kuiondoa timu ya Wakubeti FC kwa kuitandika bao 4-3 na kutinga nusu fainali katika hatua ya robo fainali iliyochezwa uwanja wa Sabasaba huku Santos FC nayo ikiambulia kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Mawingu FC katika hatua hiyo.

Timu nyingine zilizofika hatua hiyo ya robo fainali ni pamoja na Wakushi FC itayocheza na G-7 huku Obama FC ikipimana ubavu na timu ya Walabata FC katika hatua hiyo ya robo fainali.

Kwa mujibu wa Denis alisema kuwa mshindi wa kwanza atakabidhiwa seti moja ya jezi wakati mshindi wa pili akipata mipira miwili huku mshindi wa tatu akiondoka na mipira miwili na mfungaji bora yeye atakabidhiwa pea moja ya jezi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: