Kivuko kikubwa cha MV Magogoni kinachofanya safari zake kati ya Kivukoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kimekosa muelekeo majini katika bahari ya Hindi kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi.
Wananchi wakilitazama Mv. Kigamboni baada ya kupoteza mwelekeo na kushindwa kushusha abiria na magari baada ya kutaka kushusha Abiria na magari upande wa Kigamboni
Baada ya kupakia Abiria na magari upande wa kigamboni likiwemo gari maalumu la kubebea wagonjwa lilifanikiwa kutoka upande wa kigamboni na lilipofika jirani na gati upande wa Magogoni lilipoteza mwelekeo kwa dakika kadhaa hatimaye kushusha upande wa magogoni. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

0 comments:
Post a Comment