Na FREDY PASCHAL.
Ramadhani A. Masanja"Banza Stone" pichani kwa mujibu wa kaka yake Jabir alizaliwa tarehe 20/10 /1972 na atazikwa katika makaburi ya Sinza leo majira ya saa 10 Jijini Dar es Salaam.
Alisoma katika shule ya msingi Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam na kupata elimu ya muziki katika jumba la utamaduni la watu wa korea.
Alipitia katika bendi ya african stars,TOT Bendi, Bambino Sound ,Extra Bongo na kwa muda mfupi ktk Bendi ya Rungwe, atakumbukwa kwa tungo zake nzuri kama Hujafa Hujasifiwa, Mtu Pesa, Aungurumapo Simba 1&2, Kumekucha, Mtaji wa Masikini, Faksafa ya Mapenzi, Jahazi, Tushirikiane, Mpenzi toka, Euro na nyingine nyingi.
Banza alikua akiugua mrefu hadi jana tarehe 17/07/2015 alipotangulia mbele ya haki nyumbani kwake Sinza Kijiweni jirani na Vatican City, Banza ameacha mtoto mmoja Hajji Ramadhan Masanja na anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam saa 10 alasiri.

0 comments:
Post a Comment